Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akimkaribisha Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczyński katika Ofisi Ndogo za Wizara, Jijini Dar es Salaam



Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczyński akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk wakati wa maongezi yao yaliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara, Jijini Dar es Salaam



Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akimsisitizia jambo Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczyński wakati wa maongezi yao katika Ofisi Ndogo za Wizara, Jijini Dar es Salaam



Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akimkabidhi Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczyński zawadi ya kinyago

…………………………………………………….

Na Mwandishi wetu, Dar

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) amekutana na kumuaga Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczyński baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini.

Akiongea wakati wa kumuaga Balozi wa Vatican jana jioni katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam, Balozi Mbarouk amempongeza Balozi Solczyński kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kudumisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican na Tanzania.

Pamoja na mambo mengine, Balozi Mbarouk amemuahidi Askofu Mkuu Solczyński kuwa Tanzania na Vatican zitaendelea kuhimiza amani na utulivu katika masuala yenye changamoto mbalimbali ili kuwezesha uwepo wa amani na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Baba Mtakatifu katika kulinda Amani na usalama duniani kote.

Kwa upande wake Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Marek Solczynski, amesema kuwa Vatican itaendelea kuimarisha mahusiano yake ya kidiplomasia na Tanzania kwa masuala yenye maslahi ya amani na utulivu pamoja na haki na utu.

“Tumeongelea masuala mbalimbali katika kukuza diplomasia yetu na tumekubaliana kwa pamoja kudumisha amani na usalama duniani ili kuweza kuchagiza maendeleo endelevu kwa pande zote mbili,” amesema Askofu Mkuu Solczynski.

Balozi wa Vatican nchini Askofu Mkuu Marek Solczyński aliwasili nchini Tanzania Julai 12, 2017.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...