Na Janeth Raphae-Michuzi Tv Dodoma

MAMLAKA ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji Nchini EWURA imetangaza kushuka kwa bei za rejareja za mafuta ya Petrol,Dizell na mafuta ya taa yaliyopokelewa kupitia bandari ya Dar es salaam zimepungua kwa Sh 21 Lita petrol na Sh 44 mafuta ya taa huku mafuta ya dizeli yakipanda kwa Sh 13 kwa Lita.

Hayo yameelezwa Leo Jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo,Mhandisi Godfrey Chibulunje wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu mwenendo wa bei za mafuta nchini.

Hata hivyo bei za rejareja za mafuta ya Petroli na Dizeli kwa mikoa ya kusini (MTWARA, LINDI NA RUVUMA) zitaendelea kuwa zile zilizotangazwa katika toleo la Januari 5,2022,ikisababishwa na kutokuwepo kwa Shehena ya mafuta iliyopokelewa kupitia bandari ya Mtwara kwa mwezi Januari.

Katika hatua nyingine Chibulunje amesema kutokana na ufuatiliaji wa mwenendo wa beinza mafuta katika soko la Dunia ,kuna uwezekano mkubwa wa kuongezeka kwa bei za mafutakwa mwezi Machi na Aprili 2022.

Pamoja na hayo ,EWURA inaendelea kufuatilia mwenendo huo kwa karibu ili kuishauri Serikali hatua za kuchukua katika harakati za kupunguza makali ya be za mafuta nchini.

Katika kuhakikisha kunakuwa na ushinda katika Bei zinazoanza kutumika kesho ununuaji wa mafuta kutoka kwenye maghala Sasa kutakuwa na Bei mbili ambazo ni Bei Kokomo ambayo muuzaji hatatakiwa kuzidisha na Bei ya chini ambayo vilevile muuzaji hatakiwi kushuka zaidi.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...