Na Mwandishi wetu, Simanjiro
KIKUNDI
cha Faraja cha Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,
kimekarabati darasa moja la shule ya msingi Mirerani kwa gharama ya
shilingi milioni 1.6.
Katibu
wa Faraja, Lidya Mollel akisoma taarifa wakati wa kukabidhi darasa hilo
kwa Diwani wa kata ya Endiamtu Lucas Zacharia amesema waliamua
kulikarabati kama hisani kwa jamii.
Mollel
amesema ili kuunga mkono jitihada za dhati za Rais Samia Suluhu Hassan
ya ujenzi wa madarasa katika shule mbalimbali hapa nchini nao wakaiga
jambo hilo la maendeleo.
Amesema
kikundi hicho huwa wanakutana mara moja kwa mwezi kwenye shule hiyo
ndiyo sababu wakakarabati daraja moja la shule hiyo ya msingi Mirerani.
Amesema
ukarabati uliofanyika ni kuweka sakafu, kupiga plasta ndani sehemu zote
zilizobomoka, kupiga puchi ya nje na ndani, ukuta wa ndani wa darasa
hilo na kupiga rangi ndani.
“Tunamshukuru
mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mirerani Tunisia kwa ushirikiano
aliotupatia na kukubali ombi letu la kuruhusu kufanyia vikao hapa
shuleni,” amesema Mollel.
Diwani
wa kata ya Endiamtu Lucas Chimba Zacharia amewapongeza wanachama wa
kikundi cha Faraja kwa kufanikisha ukarabati wa darasa moja la shule ya
msingi Mirerani kwa gharama zao.
“Ninawashukuru
na kuwapongeza wanachama wa Faraja kwa kuamua kuiunga mkono Serikali na
kukarabati darasa moja ambalo lilikuwa linawapa wakati mgumu wanafunzi
kusoma,” amesema Luka.
Mwalimu
mkuu wa shule ya msingi Mirerani Tenisia Katukuru aliwapongeza
wanachama wa Faraja kwa kukarabati darasa hilo moja la shule yake kwani
hivi sasa wanafunzi wanasoma vizuri.
“Awali
darasa hilo lilikuwa limechakaa hata kuvuta dawati ilikuwa shida kwani
kulikuwa na mabonde mabonde hivyo wanafunzi kutokuwa na wasaa mzuri wa
kusoma,” amesema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...