Na Farida Said, Michuzi Tv.

Magari ya abiria, mizigo na magari madogo yanayofanya safari zake katika mikoa ya nyanda za juu kusini , Morogoro na Dar es salaam yamekwama kwa zaidi ya saa sita katika eneo la Doma lililopo Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kufuatia mvua kubwa kunyesha usiku wa kuamkia February mosi na kusababisha daraja la Doma kufunikwa na magogo kisha maji kupita juu ya daraja na kuharibu baadhi ya maeneo ya daraja hilo.

Michuzi Blog imefika katika eneo hilo na kushuhudia maji yakiwa yanapita juu ya Daraja huku magari yanayopita barabara ya Morogoro Iringa yakiwa yameshindwa kupita ambapo mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa hali hiyo imetokana na mvua kubwa ambayo imenyesha usiku wa kuamkia February mosi.

Aidha wamesema kuwa kufurika kwa maji kwenye daraja hilo ni kutokana na magogo makubwa ambayo yamesombwa kutoka juu milimani, hivyo kupekea kuziba baadhi ya mapitio ya maji katika daraja hilo.

Kufuatia tukio hilo wakala wa barabara nchini TANROADS Mkoa wa Morogoro umefika kwenye daraja hilo ili kutafutia ufumbuzi wa changamoto hiyo ambapo meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro Mhandisi Alihanuswe Kyamba amesema kwa sasa wanatafuta ufumbuzi ili magari yaweze kupita.

Kutokana na hali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Muslim amelazimika kufika katika eneo hilo, ambapo amesema hakuna madhara yoyote katika daraja hilo na wananchi kwa ujumla.

Hata hivyo baada ya maji kupungua Kamanda Muslimu kwa kushirikiana na TANROADS Mkoa wa Morogoro wameruhusu magari kupita katika daraja hilo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...