Baadhi
ya Wasanii waliokidhi vigezo vya kisheria na kukidhi masharti ya
kupata mgawo wa mirabaha wameendelea kumiminika katika ofisi za Taasisi
ya Hakimiliki (COSOTA), kuanzia jana Januari 31,2022, kuwasilisha
taarifa zao za kibenki na kukamilisha taratibu za msingi ili kuweza
kukamilisha zoezi la ulipwaji wa mirabaha yao.
Miongoni mwa Wasanii hao ni Ambwene Yesaya (AY), Farid Kubanda (Fid Q), Chege Chigunda pamoja na Meneja wa kundi la Mabantu.
Pamoja
na hayo Wasanii hao wamemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuweka msisitizo katika kusimamiwa
kwa Hakimiliki za Wasanii pamoja na kuhakikisha wasanii hao wanapata
mgao wa mirabaha kwa kazi zao zinazotumika katika maeneo mbalimbali ya
biashara.
Halikadhalika wameipongeza COSOTA
kwa kuwalipa mirabaha kwani ni muda mrefu hawajapata mirabaha na pia
hawajawahi kupata gawio kubwa kama ilivyo katika mgao huo wa sasa.
Kwa mujibu wa sheria wasanii wanaolipwa mirabaha ni wale
ambao
wamejisajili Cosota kazi zao na pia kazi hizo zimethibitika kuzumiwa
kibiashara (economic use) kama vile muziki kupigwa katika vituo vya
redio au kazi yoyote ya fasihi mfano kitabi kuingizwa katika matumizi ya
kuigizwa katika filamu ya kibiashara.
“Mrabaha
si mbadala wa mauzo ya kazi ya msanii bali ni kama fidia anayopewa
mbunifu kwa kazi yake aliyoiingiza sokoni kisha kutumiwa na watu wengine
kibiashara. Iwapo kazi ya msanii haijatumiwa kibiashara hata kama
ameiuza na iko sokoni kwa wingi basi hana haki ya mrabaha na wingi wa
kutumika kazi ya mtu ndio unaotofautisha ukubwa wa mapato kati ya mtu
mmoja hadi mwingine,” amefafanua Ofisa wa Cosota.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...