Na John Walter-Babati

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara Anna Mbogo, amesema atawachukulia hatua za kisheria watendaji wa kata na vijiji ambao wameshindwa kuitisha vikao vya kisheria kwenye maeneo yao.

Kauli hiyo ameitoa Februari 4,2022 katika kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichofanyika leo ambapo amesema kuna shughuli za kimaendeleo zinakwama kutokana na watendaji hao kutoitisha vikao hivyo.Hayo yanajiri kukiwa na taarifa kuwa Halmashauri hiyo yenye vijiji 102,vijiji 28 pekee ndio ambavyo vinaonekana vimetimiza wajibu wao wa kuitisha vikao vinavyohitajika kufanyika kwa mujibu wa sheria.

Amewatahadharisha Madiwani wasilalalamike kwa uamuzi atakaouchukua juu ya watendaji wasiotimiza wajibu wao kama utaratibu unavyoelekeza.
Katika hatua nyingine,madiwani hao wakizungumza katika baraza hilo wamesema wapo baadhi ya watendaji katika kata na vijiji hawaishi eneo la kazi na badala yake wanaishi mijini na wakati mwingine kukosekana kabisa katika ofisi zao.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Babati Mheshimiwa John Noya amesema watendaji wasiotimiza wajibu wao wanapaswa kuwajibishwa kwa kuwa wanakwamisha shughuli za serikali kufanyika kwa wakati.

Kwa mujibu wa taratibu kikao cha kisheria cha Halmashauri ya Kijiji kinapaswa kuketi kila mwezi,mkutano mkuu kila baada ya miezi mitatu yaani robo mwaka.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...