BENKI ya Biashara ya NBC imejizatiti katika uwekezaji wa sekta ya Kilimo takribani Bilioni 100 kwa mwaka 2022 na kuwataka wateja wao kuendelea kuwaamini kwenye utoaji wa huduma za kifedha na mikopo
NBC imekutana na wateja wao wakubwa na wawekezaji ili kujadiliana masuala mbalimbali ya kimaendeleo na Wawekezaji wakubwa wanaopata huduma katika benki yao.
Katika hafla hiyo , NBC imewataka wafanyabiashara hao kuendelea kuwaamini na kuendelea kutumia benki hiyo inayomsikiliza mteja.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo,Mkurugenzi. Wa Kitengo cha Wafanyabiashara wakubwa na Wawekezaji. James Metaron amesema wanafuraha kuona wana wateja wao ambao wameshirikiana nao katika huduma za kibenki kwa takribani miaka 20 na wanaendelea kunufaika kibiashara.
Amesema, benki ya NBC imejikita zaidi katika kuhudumia wateja wote hususani wakulima kwa kuwawezesa kuwaamini ha kupata fedha za kununua mazao kutoka kwa vyama vya ushirika, kuandaa shamba na hadi mitaji ya biashara.
“Tunatoa huduma za kifedha kwa wateja wakubwa, kwa upande wa Kilimo tumekuwa tunawasaidia katika kununua mazao kutoka kwa vyama vya ushirika na hata muda mwingine tunampatia mteja fedha kwa ajili ya kuandaa shamba lake kabla ya kulima,”
Aidha, amesema NBC imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Kilimo kinakua na kupitia benki yao na inawahamasisha wateja wadogo na wakubwa kujiunga kutokana na uzoefu mkubwa waliokuwa nao.
“Tunafanya biashara katika sekta zote ila Tumejikita zaidi kwenye kilimo ili kusapoti wateja wetu na hata kwa wafanyabiashara wakubwa,”
“Kwa mwaka 2022 benki ya nbc Imejizatiti kwa kuwekeza fedha nyingi takribani Bilion 100 ili kuwasaidia wakulima kununua na kusafirisha mazao ndani na nje ya nchi,”
Naye Keneth Woiso ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Woiso Inayoshughulika na masuala ya kutengeneza bidhaa asilia za ngozi amesema akaunti yake ya na NBC ina umri wa kijana.
Amesema katika kipindi chote NBC wamekuwa na msaada mkubwa sana kwao na wameweza kushirikiana vizuri pindi anapokuwa amekwama kwenye masuala ya kibiashara kupitia kampuni yake ya Woiso.
Aidha, ameishukuru NBC kwa kazi na jitihada wanazofanya kwa wajasiriamali wakubwa na wadogo pindi wanapotaka huduma za kifedha kama vile mkopo na elimu ya biashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara NBC Theobadi Sabi (wa pili kulia) akizungumza na baadhi ua wateja wakubwa na wawekezaji wakati wa hafla ya Chakula cha Usiku kwa lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara NBC Theobadi Sabi (kushoto) akizungumza na baadhi ua wateja wakubwa na wawekezaji wakati wa hafla ya Chakula cha Usiku kwa lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...