Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) leo imekabidhi msaada wa samani ya Meza kumi (10) na Viti kumi (10) kwa ajili ya matumizi ya Walimu katika shule ya msingi Kinyerezi Jica iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya TAA ya kurudisha kwa Jamii (Corporate Social Responsibility).

 
Akikabidhi Samani hizo Mwenyekiti wa kamati ya kurudisha kwa jamii (CSR) Bw, Maxmilian Mahangila kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAA amesema, dhumuni la msaada huu ni Kuwawezesha waalimu kuwa na mazingira mazuri ya kufanyia kazi ili waweze kufundisha wanafunzi kwa viwango vya ubora Zaidi, lakini pia kujenga mahusiano mema kwa jamii nzima.
 
 ‘’ Hawa wanafunzi mnaowafundisha hapa tunawategema sana kuwa viongozi na wafanyakazi wa baadae serikalini na katika sekta binafsi, hivyo kutoa msaada huu leo ni kuwawezesha walimu muwafundishe vyema ili waje wasaidie Taifa letu, kwani Samani hizi tunazotoa zinawasaidia katika kazi zenu mbalimbali za kuandaa masomo ya kufundisha, kusahisha kazi za wanafunzi na kazi nyingine nyingi ambazo waalimu mnakuwa nazo’’, alisema Bw, Mahangila.
 
Naye Mkuu wa shule,Bw. Baraka Baltazar ameishukuru Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) kwa kusaidia Samani ambazo ilikuwa ni hitaji la muda mrefu na muhimu kwa Waalimu wa shule kupata Meza na Viti ili visaidie katika Matumizi ya shule na kupunguza changamoto katika mazingira ya ufundishaji.
 
‘‘Tunashukuru sana kwa msaada mkubwa mliotupatia umesaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa meza na viti kwa waalimu hivyo ufanisi wa utendaji kazi katika mazingira bora utaongezeka’’ alisema Mkuu wa shule.
 
Aidha Bw Baltazar ameainisha changamoto kadhaa ambazo bado zinaikabili shule yake ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa maji kutokana na miundombinu kutokuwa Rafiki hivyo kuitaji kisima pamoja na matanki mawili ya kuhifadhia maji ya lita 5000, Maktaba kwa ajili ya waalimu na wanafunzi kujiongezea maarifa pamoja na vifaa vya Tehama kutokana maendeleo ya teknolojia kwa hivi sasa.
 
Shule ya msingi Kinyerezi Jica ilianzishwa Januari 2016 baada ya kugawanywa kutoka shule ya msingi Kinyerezi kutokana na wingi wa wanafunzi waliokuwepo. Shule hii inakua kwa kasi ambapo kwa sasa inajumla ya madarasa 18 na idadi ya wanafunzi imefikia wanafunzi 1538 na walimu 51 ukilinganisha na hali iliyokuwepo wakati shule inaanzishwa ikiwa na madara 6, wanafunzi 587 na waalimu 13.
 
Shule ya msingi Kinyerezi Jica ni moja ya shule inayofanya vizuri kitaaluma mwaka hadi mwaka katika kata ya kinyerezi, Halmashauri ya jiji la Dar es saalam.
Wakati huohuo Katika kutambua mchango uliotolewa na TAA uongozi wa shule ya msingi Kinyerezi Jica umeipatia TAA cheti cha kutambua mchango uliotolewa ‘’ Certificate of Appreciation’’ na kuiomba TAA kuwa Mlezi wa shule ya msingi Kinyerezi Jica.
Mwenyekiti wa Kamati ya TAA ya  kurudisha kwa jamii (CSR) kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania  (TAA) Bw. Maxmilian Mahangila katikati akikata utepe kuashiria  makabidhiano ya msaada wa samani za meza 10 na viti 10 kwa ajili ya matumizi ya  ofisi ya waalimu katika shule ya Msingi Kinyerezi Jica uliotolewa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania mapema leo.
Afisa Elimu kata ya Kinyerezi Bi, Radhia Mfalingundi akimkabidhi Cheti cha kutambua Mchango wa msaada kutoka  TAA (Certificate of Appreciation) Bw. Maxmilian Mahangila, kwa niaba ya shule ya Msingi Kinyerezi Jica mara  baada ya kutoa Msaada wa samani  katika shule hiyo.
Picha ya pamoja kati ya Uongozi na waalimu wa shule ya Msingi Kinyerezi Jica pamoja na wawakilishi kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania mara baada ya kukabidhi msaada wa Samani za Meza na viti kwa shule hiyo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...