Na Pamela Mollel,Arusha
Jumla ya wananchi 126 kutoka kata ya Terat na Muriet jijini Arusha wanufaika na programu mahususi ya kumaliza malipo ya shilingi elfu ishirini na saba baada ya bei mpya kutangazwa kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)Mkoani Arusha
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Arusha Herini Mhina akiwa katika ziara ya kuwaelimisha wananchi juu ya program hiyo alisema kuwa Kata ya Muriet na Terat ndani ya wiki moja zoezi la kuwafungia umeme kwa wale waliolipia pamoja na kukamilisha usambazaji wa nyaya za umeme ndani ya nyumba zao watapata huduma hii
"Leo tumezindua rasmi program mahususi ya kumaliza malipo ya shilingi 27 yaliyofanyika baada ya bei mpya kutangazwa na hapa Muriet wateja ni 73 Terat 53"alisema Mhina
Alisema kuwa program hiyo ni endelevu itahusisha maeneo mengine yenye wateja wengi ikiwemo Wilaya ya Arumeru lengo likiwa ni kuhakikisha mteja anafungiwa umeme ndani ya siku 7 baada ya kufanya malipo.
Shirika hilo lina mikakati mipana ya kuhakikisha inaweka mfumo wa ujazaji fomu katika mtandaoni ili kuepuka usumbufu wa hapa na pale kwa mteja pindi anapotaka huduma ya kuunganishiwa umeme
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mrisho Gambo katika ziara hiyo amelipongeza shirika hilo kupitia Waziri wa Nishati Mhe.Januari Makamba na menejimenti yote kwa kasi waliyoianza kuionyesha katika jimbo la Arusha mjini kwa ajili ya kushughulikia changamoto za wananchi.
Aliwataka wananchi wa jimbo la Arusha hususani waliopo katika Kata ambazo programu hiyo itatekelezwa kuhakikisha wanafanya matayarisho yote mahususi ikiwa ni pamoja na kutandaza nyaya katika nyumba zao kwa mujibu wa taratibu zote sambamba na kufanya malipo ya elfu ishirini na saba ili waweze kupata huduma hiyo ya umeme.
Gambo alisema kuwa hatua ya TANESCO kuanza kutandaza nguzo katika eneo la Olepolosi Kata ya Terati ni hatua nzuri naya kupongezwa kwani tangu nchi ipate uhuru eneo hilo lilikuwa na umeme mkubwa amnapo umeme mdogo halikuwahi kuwepo kwa wananchi hivyo ahadi zilizotolewa za kutekeleza mipango yao ni ahadi nzuri na yakupongezwa
Mzee Tobiko wa jamiii ya kifugaji kutoka kijiji cha Nadosoito wakati akiwasilisha kero zao ameiomba Tanesco kutotumia siasa katika utoaji wa huduma za umeme kwa wananchi kwani imekuta ni kero kubwa kwa wananchi kukaa muda mrefu bila kuunganishiwa umeme baada ya kufanya malipo.
"Niwapongeze sana Tanesco kwa kazi kubwa wanayofanya bila kumsahau Mbuge wetu Gambo amefanya mambo makubwa sana na amefanya eneo hili kutambulika rasmi"alisema Mzee Tobiko
Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nadosoito kata ya Muriet kuhusu programu hiyo na kuwataka wachangamkie fursa kwa kukamilisha maliopo pamoja na kuweka nyaya za umeme katika nyumba zao ili waweze kupata huduma
Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha Mhandishi Herini Mhina akizungumza na waandishi wa habari katika kijiji cha Nadosoito kata ya Muriet kuhusu programu mahususi ya kumaliza malipo ya shilingi elfu27 baada ya bei mpya kutangazwa
Meneja wa Tanesco mkoa wa Arusha mhadisi Herini Mhina akiteta jambo na mzee Tobiko
Diwani wa kata ya Terat Julius Senina akizungumzia katika mkutano wa wananchi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...