Wizara ya Maliasili na Utalii imezindua namba za kijeshi za magari, Mitambo, na Vyombo vingine vya moto vya Jeshi la uhifadhi wa wanyamapori na misitu Tanzania.
Uzinduzi huo umefanyika leo Februari 04, 2022 Mtumba Dodoma katika ofisi za Maliasili na utalii
Akizungumza na waandishi wa habari Mara baada ya uzinduzi huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt Francis Michael amesema sababu kubwa ya kuanzishwa kwa jeshi la uhifadhi ni kuimarisha ULINZI wa rasilimali za wanyamapori na misitu na zile zinazoambatana nazo, pia ni kufuatia kuongezeka kwa ujangili wa wanyamapori wakubwa hususani tembo na faru na kuongezeka kwa uvunaji haramu wa mazao ya misitu katika kipindi Cha miaka ya 2000.
"Baada ya uzinduzi wa Jeshi la Uhifadhi (JU) Mwaka 2018, Wizara imekamilisha maandalizi ya nyenzo na vitendea kazi mbalimbali vitakavyosaidia utekelezaji wa mfumo wa kijeshi. Baadhi ya vitendea kazi hivyo ni pamoja na kanuni za Jeshi la Uhifadhi, Amri za jumla za Jeshi la Uhifadhi (General Orders), mitaala ya Jeshi la Uhifadhi, vyuo vya kutolea mafunzo kwa Maafisa na askari wake pamoja na namba maalumu zitakazokuwa zinatumiwa na magari, mitambo na vyombo vingine vya moto vinavyomikikiwa na Jeshi la Uhifadhi" - Amesema Katibu Mkuu Dkt Michael.
Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Maliasili na Utalii amezitambulisha namba hizo maalumu za usajili za kijeshi zitakazokuwa zinatumiwa na Jeshi la Uhifadhi Wanyamapori na Misitu ambazo zitasomeka Kama ifuatavyo:-
CC 01 - Gari ya Kamishina wa Uhifadhi Ngororo.
CC 02 - Gari ya Kamishina wa Uhifadhi TANAPA.
CC 03 - Gari ya Kamishina wa Uhifadhi TAWA.
CC 04 - Gari ya kamishina wa Uhifadhi TFS.
Wakati huo huo Dkt Michael amesema magari na Vyombo vya moto vitasimeka:-
NGORORO 01 JU 00001 na kuendelea.
TANAPA 02 JU 0001 na kuendelea.
TAWA 03 JU 0001 na kuendelea na TFS 04 JU 0001 na kuendelea.
Hata hivyo Mara baada ya uzinduzi wa namba hizo Wizara hiyo ya Maliasili na Utalii imepokea na kutoa magari kumi na tank (15) ya jeshi la uhifadhi yatakayotumika na TFS.
Magari hayo yamenunuliwa kwa fedha za Serikali Kama sehemu ya kuimarisha utendaji wa Jeshi hilo katika kusimamia rasilimali za misitu na nyuki.
Magari hayo yatagawanywa kwa matumizi katika Wilaya za Mlele, Mapanda, Songea, Tunduru, Longido, Rombo, Serengeti, Manyoni, Bahi, Mvomero, Kibaha, Mufindi na Chunya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...