Benki ya Exim Tanzania imekabidhi msaada wa madawati 100 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 mkoani Mbeya ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa benki hiyo wa kutoa msaada wa madawati 1000 katika mikoa mbalimbali hapa nchini ili kuchangia utoaji wa elimu bora kupitia mpango wake wa uwajibikaji wa Jamii (CSR) ujulikanao kama Exim Cares.

Madawati hayo yalikabidhiwa na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano Benki ya Exim Bw Stanley Kafu kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw Juma Zuberi Homera wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa huyo Mkoa mapema hii leo. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wengine waandamizi wa Mkoa huo akiwemo Katibu Tawala wa mkoa huo Bi Angelina Lutambi .

Akizungumza mara tu baada ya kupokea msaada huo Bw Homera pamoja na kuishukuru benki ya Exim kwa kutoa msaada huo, alisema msaada huo unakwenda sambamba na jitihada za serikali za kuboresha hali ya elimu mkoani humo na kwamba msaada huo utasaidia kupunguza uhitaji wa madawati unaotokana na miradi mingi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa inayoendelea mkoani humo.

"Msaada huu utasaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa madawati katika baadhi ya shule zetu…tunashukuru sana wenzetu wa Benki ya Exim kwa msaada huu na tunaomba muendelee kusaidia kwenye maeneo mengine pia ikiwemo sekta ya afya . Mheshimiwa Rais anapambana kutafuta fedha kwa ajili ya miradi mikubwa inayoendelea nchini hivyo ni jambo linalotia moyo kwake kuona wadau kama mabenki mkiendelea kumuunga mkono " Alisema.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Katibu Tawala wa Mkoa Mbeya Bi Lutambi alizitaja baadhi ya shule zitakazonifaika na msaada huo kuwa ni Shule ya Msingi Mwenge na Shule ya Msingi Jitegemee za jijini humo zinazokabiliwa na uhaba mkubwa wa madawati.

Kwa upande wake Bw Kafu alisema kuwa benki hiyo imejitolea kusaidia katika kuboresha ustawi wa jamii kupitia misaada ya kijamii ikiwemo elimu na kwamba wameguswa sana na suala la changamoto ya madawatikwenye baadhi ya maeneo hapa nchini sababu iliyosababisha wao kuchukua hatua hiyo ili kuboresha zaidi sekta hiyo muhimu

"Ni furaha kwetu kuwa sehemu ya kutatua changamoto kwenye sekta muhimu kama hii. Huu ni mwendelezo tu bado tunaendelea na mikoa mingine kwa kuwa lengo ni kutoa msaada wa madawati 1000 kama tulivyomuahidi Mh Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati tunazindua mpango huu Mkoani Mtwara mwishoni mwa mwaka jana,’’ alisema Bw Kafu huku akiitaja mikoa mingine ambayo imekwisha nufaika na mpango huo kuwa ni Mtwara na Mwanza.

Alishauri pia wanafunzi na walimu watakaonufaika na msaada huo kutunza madawati hayo ili yaweze kutumika kwa muda mrefu na hivyo kusaidia walengwa wengi zaidi.






Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano Benki ya Exim Bw Stanley Kafu (kushoto) akikabidhi madawati 100 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw Juma Zuberi Homera ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa benki hiyo wa kutoa msaada wa madawati 1000 katika mikoa mbalimbali hapa nchini ili kuchangia utoaji wa elimu bora kupitia mpango wake wa uwajibikaji wa Jamii (CSR) ujulikanao kama Exim Cares wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa huyo Mkoa mapema hii leo. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa Mbeya Bi Angelina Lutambi.




Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw Juma Zuberi Homera (wa pili kulia) na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano Benki ya Exim Bw Stanley Kafu (wa pili kushoto) wakiwa wameketi kwenye moja ya madawati 100 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya kusaidia kuchangia utoaji wa elimu bora mkoani humo kupitia mpango wake wa uwajibikaji wa Jamii (CSR) ujulikanao kama Exim Cares wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa huyo Mkoa mapema hii leo.




Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano Benki ya Exim Bw Stanley Kafu (katikati) akizungumza na viongozi wa mkoa wa Mbeya wakati akikabidhi madawati 100 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw Juma Zuberi Homera ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa benki hiyo wa kutoa msaada wa madawati 1000 katika mikoa mbalimbali hapa nchini ili kuchangia utoaji wa elimu bora kupitia mpango wake wa uwajibikaji wa Jamii (CSR) ujulikanao kama Exim Cares wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa huyo Mkoa mapema hii leo.




Akizungumza mara tu baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw Juma Zuberi Homera (Kulia) pamoja na kuishukuru benki ya Exim kwa kutoa msaada huo, alisema msaada huo unakwenda sambamba na jitihada za serikali za kuboresha hali ya elimu mkoani humo na kwamba msaada huo utasaidia kupunguza uhitaji wa madawati unaotokana na miradi mingi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa inayoendelea mkoani humo.




Akizungumza kwenye hafla hiyo Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Bw Ernest Hinjuu (Kulia) alizitaja baadhi ya shule zitakazonifaika na msaada huo kuwa ni Shule ya Msingi Mwenge na Shule ya Msingi Jitegemee za jijini humo zinazokabiliwa na uhaba mkubwa wa madawati.




Baadhi ya wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Mwenge na Shule ya Msingi Jitegemee za jijini Mbeya wakiwa wameketi kwenye madawati hayo.





Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw Juma Zuberi Homera (wa TATU kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa mkoa huo pamoja na wawakilishi wa Benki ya Exim wakati wa hafla hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...