Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa ameagiza shule zote wilayani humo kufundisha neno la upendo kwa wanafunzi kwa dakika kumi kabla ya kuingia darasani ili kuondoa roho ya ukatili inayosababisha mauaji mkoani Njombe.
Mkuu huyo wa wilaya katika ibada ya maombi ya Dunia iliyofanywa na umoja wa wanawake wa madhehebu ya kikrito mkoani Njombe iliyofanywa katika kanisa la Moravian Mjini Njombe, amesema ametoa agizo hilo kwa kamati ya ulinzi na usalama ili kujenga upendo kwa jamii kuanzia kwa watoto.
“Nimetoa agizo kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya,watoto wote dakika kumi kabla ya kuingia darasani shule zote zifundishe neon la upendo.Hata kama sitafanikiwa mwaka huu ninaamini kama jambo hili litadumu tutaweza kuibadirisha Njombe”alisema Kissa Kasongwa
Kwa upande wake mwenyekiti wajumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Njombe Betreace Malekela ametoa wito kwa wanawake kuendelea kuomba ili kulipigania taifa na wilaya
ya Njombe.
“Wanawake tuendelea kusimama na kumuombea Rais wetu,tumuombee spika na tumuombee mkuu wetu wa wilaya ili taifa liende na wilaya yetu iende”alisema Betreace Malekela
Akizungumza kwa niaba ya umoja wa wanawake wa madhehebu ya kikrito mkoani Njombe Bi, Roida Mlele ambaye ni mwenyekiti kutoka kanisa Anglikana amesema licha ya akina mama kuwa wamoja katika maombi lakini wameendelea na shughuli zao za kuinua uchumi wa familia na wilaya.
“Pia kina mama licha ya kushirikiana kwenye shida mbali mbali lakini wanajishughulisha na shughuli za kuinua uchumi wao kama kilimo,biashara na kazi za ofisini”alisema Bi,Roida Mlele.
Baadhi ya wanawake wakiwa kwenye maombi ya kidunia yaliyofanywa na umoja wa wanawake wa madhehebu ya kikrito mkoani Njombe
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...