Na Mwandishi Wetu,Pwani

MKUU wa Wilaya ya Kibaha Sara Msafiri ametoa maelekezo kwa Shirika la Umeme Tanesco kuhakikisha wanatoa taarifa kwa wamiliki wa Viwanda kabla ya kukata umeme kuepusha usumbufu na uharibifu wa mashine unaoweza kutokea.

Sara ametoa maelekezo hayo jana alipofanya ziara ya siku moja kukagua viwanda na kuongea na wawekezaji kujua changamoto wanazokabiliana nazo ili zitafutiwe ufumbuzi.

Akiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha katika kiwanda cha Pamba za kutengenezea mito na magodoro, Nondo na kiwanda cha kuzalisha vifaranga na chakula cha mifugo, Sara alipokea changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara ambao unasababisha kusimamisha uzalishaji huku wengine wakihofia kuharibika kwa mashine kutokana na hali hiyo.

Amewataka Tanesco kufanya matengenezo kwenye maeneo yanayoelezwa kuwa na uchakavu wa miundombinu ili kuwaondolea wawekezaji vikwazo vya kuendelea na shughuli za uzalishaji

Kwa mujibu wa Sara amesema Serikali inaweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji ili waweze kuzalisha kwa mqlengo waliyojiwekea hivyo ziara hiyo inalenga kuleta suluhisho la vikwazo wanavyokabiliana navyo.

Aidha Sara alitoa maelekezo kwa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salam kuhakikisha ifikapo April saba wawe wamekutana na kiwanda cha kutengeneza chakula cha mifugo na kuzalisha vifaranga na mayai kujadiliana namna ya kuwaunganishia maji.

Akitoa taarifa kwa Mkuu wa wilaya ,mwakilishi wa kiwanda hicho cha kutengeneza chakula cha mifugo Animal care Company Idd Nasibu alisema kwasasa wameshatoa ajira 225 na kwamba bidhaa zao wanasambaza katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Tanga na Zanzibar ambapo lengo lao ni kufikia nchi nzima.

Alieleza pia vikwazo wavyokumbana navyo ni pamoja na barabara, umeme usio wa uhakika na maji ya DAWASA.

Nasibu amewataka vijana kujikita katika shughuli za ufugaji ambazo zinaweza kuwainua kiuchumi badala ya kuendelea kuona kazi sahihi ni kuendesha boda boda pekee.

Nasibu amesema ufugaji ni sehemu ya ajira ambayo vijana wakijikita huko wanaweza kunufaika zaidi badala ya kusimamia eneo la bodaboda ambalo baadhi yao wamelionq ni sehemu ya ajira zao baada ya kukosa sehemu nyingine.

Amesema kwasasa mbali ya kusambaza bidhaa hizo katika maeneo mbalimbali pia wanatoa mafunzo kwa vikundi na watu mbalkmbali wanaotaka kufuga na madaktari wa kiwanda hicho wamejenga utaratibu wa kutembelea maendeleo yao.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...