NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Hussein Ali Mwinyi, amewataka Wanaccm na wananchi kwa ujumla kuendelea kuenzi amani,utulivu,umoja na mshikamano uliopo nchini.

Rai hiyo ameitoa katika kongamano la uzinduzi wa wiki ya Umoja wa Wazazi wa CCM Kitaifa, iliyofanyika katika ukumbi wa CCM Amani Mkoa, Unguja.

Dk.Mwinyi alisema maendeleo ya Zanzibar yanategemea zaidi uwepo wa amani na mshikamano hivyo kila mwananchi wana wajibu wa kuheshimu,kuthamini na kulinda amani kwa ustawi wa nchi.

Katika maelezo yake Dk.Mwinyi, alifafanua kwamba falsafa ya uchumi wa buluu (Blue Economy)inayoelekeza matumizi bora ya rasilimali za bahari ni miongoni mwa sera ya CCM iliyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020/2025 yenye lengo la kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi Zanzibar.

“Nafurahi katika moja ya mada zilizotajwa hapa ipo ya uchumi wa bluu, tusichoke na tuendelee kuelimishana pindi tunapopata fursa ya kukutana kama hivi na katika mikusanyiko mbalimbali ya kijamii. “, alisema Dk.Mwinyi.

Bado wananchi wengi hawajaelewa vizuri dhana ya uchumi wa bluu, hivyo tutaendelea kuelimishana na kutekeleza dhana hiyo kwa vitendo ili sote tuwe na uelewa wa pamoja na kusonga mbele kimaendeleo.

Akizungumzia kongamano hilo alieleza kuwa umoja wa wazazi ni jumuiya yenye historia kubwa toka enzi za ASP na TANU iliyopigania hatua mbalimbali za kimaendeleo nchini.

Alisema Kongamano hilo litumike kueleza hatua mbalimbali za mafanikio zilizofikiwa na serikali zote mbili ili Wanaccm waendelee kuunga mkono juhudi hizo.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu CCM Taifa Dk.Mwinyi, aliwataka wanaccm kuchagua viongozi waliokuwa tayari kukitumikia Chama na sio kuwagawa wanachama.

Dk.Mwinyi aliutaka umoja huo kuendelea kuongeza wanachama wapya kwani ndio mtaji imara wa CCM kisiasa katika mchakato wa uchaguzi mkuu wa Dola.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi, alisema CCM inaridhishwa na utendaji uliotukuka wa Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali mwinyi pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dk.Mabodi, alimsihi Rais Mwinyi kuendelea kuchapa kazi bila kujali vikwazo na kauli zisizofaa zinazosemwa na baadhi ya watu wasiopenda maendeleo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Mapema Katibu Mkuu wa Umoja wa wazazi Tanzania Gilbert Kalima, alisema umoja huo unatimiza miaka 67 toka kuasisiwa kwake hivyo unajivunia mambo mengi mazuri katika ukomavu wa kisiasa na ustawi wa nchi.

Alisema umoja huo utaendelea kuenzi juhudi za maendeleo zinazofanywa na serikali zote mbili pamoja na kuwalinda na kuwatetea viongozi wake ili watekeleze kwa ufanisi Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...