Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kutoa ufafanuzi kwa umma kuhusu taarifa iliyotolewa na mtandao wa Tanzania Times tarehe 3 Machi, 2022 ikieleza kuonekana kwa faru mweusi katika Hifadhi ya Taifa Nyerere.
Taarifa hiyo ambayo inaendelea kusambaa katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii sio sahihi na tunaomba ipuuzwe. Ukweli ni kwamba hakuna Faru mweusi aliyeonekana katika hifadhi ya Taifa ya Nyerere kama ilivyoripotiwa na mtandao huo.
Aidha, Wizara inasisitiza kuwa Msemaji Mkuu wa masuala ya wanyampori hapa nchni ikiwemo utoaji wa takwimu na taarifa za wanyamapori kwa umma ni Wizara ya Maliasili na Utalii na si vinginevyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...