Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Mpwapwa.

HALMASHAURI ya Wilaya ya Mpwapwa katika Mkoa wa Dodoma imesema uwepo wa mradi wa kilimo himilivu cha Mtama unaotekelezwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani(WFP) pamoja na Shirika la Farm Afrika umekuwa chachu kubwa ya kuinua vipato vya wananchi wanaojihusisha na kilimo hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari walipofika kumtembelea ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mwanahamis Ally amefafanua hatua kwa hatu namna ambavyo wakulimwa wa zao la mtama kupitia mradi huo ambavyo wameendelea kunufaika na zao hilo.

"Tunafarijika kuwa na WFP pamoja na Farm Afrika katika halmashauri kilimo cha mtama kimekuwa maarufu sana hapa kwetu lakini kimeleta tija kwa wananchi kwani kimeboresha kipato lakini kimesaidia kuongeza pato la halmashauri, ukienda kwenye jamii sasa hivi wanazungumzia WFP na Farm Afrika kwa namna gani wamenyanyua vipato kupitia zao la mtama.

"Mwaka huu mvua zilichelewa kunyesha, hivyo wengi wamelima mtama , pia wamelima kwasababu ya kuwa na uhakika wa soko baada ya kuvuna mtama , WFP na Farm Afrika wametafuta soko kwa ajili ya zao hilo na Kiwanda cha Bia cha TBL kimekuwa munuzi mkubwa wa mtama.Kwa hiyo sisi halmashauri, WFP na Farm Afrika tumekuwa kitu kimoja.

"Wote tunamkomboa mwananchi wa Mpwapwa, wote tunachangia kwenye pato la halmashauri ya Mpwapwa.Niseme tu hili zao la mtama limekuwa mkombozi mkubwa katika jamii yetu na wananchi wamekuwa mashuhuda wa manufaa ambayo yanapatikana kupitia kilimo cha mtama, "amesema.

Ameongeza kuna kikundi cha wakulima wa mtama ambao wamedhamiria kuongeza mashamba katika msimu huu wa kilimo hivyo jukumu mojawapo la halmashauri ni kuendelea kuwamasisha wananchi kulima zao hilo."Halmashauri kupitia idara ya kilimo tumeendelea kuwapa uatalaamu wakulima kuhusu kilimo na uhifadhi mazao.

"Kwasababu kulima ni mchakato unaoanzia shambani lakini kuna uvunaji bora ili mkulima anapovuna asiweke vitu ambavyo havitakiwi.Hata hivyo tumejipanga kuboresha maghala kwani tumeona wanapovuna wanakosa mahali pa kuhifadhi mazao ,kwa hiyo tutaboresha maghala kwenye maeneo husika."

Kuhusu mchango wa zao la mtama kwenye pato la halmashauri amesema kwa sasa wako kwenye uchambuzi na hatimaye watajua mtama umewaingizia kiasi gani, kwa hiyo kuanzia mwaka huu wataweka takwimu za mtama katika kuchangia pato la halmashauri.

Awali Ofisa Kilimo Mpwapwa wake Edson Kileo kutoka Idara ya amesema mradi wa kilimo himilivu cha mtama kinatekelezwa katika vijiji 51 na kata 22."Mradi huu wa kilimo himilivu cha Mtama wakati unaanza wakulima walipewa elimu na hadi sasa wapo wanuifaka 5,558 , mradi huu katika utekelezaji wake umewezesha wakulima kupata mbegu bora za mtama.Pia wakulima wameingia mkataba na TBL kwa ajili ya kununua mtama."

Ofisa wa Ufuatiliaji wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani ( WFP) akiwa na Ofisa Mawasiliano wa Shirika hilo Desta Laiza ( kushoto)wakijadiliana jambo wakati wa ziara ya kukagua mradi wa Kilimo himilivu cha Mtama.Mradi huo unatekelezwa na WFP kwa kushirikiana na Farm Afrika.
Mmoja wa maofisa wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) akiwa ameshika moja mche wa mti lishe
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...