Maadhimisho haya ya kimataifa ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 8 Machi, Siku ya Wanawake duniani ni tukio la kuimarisha dhamira ya usawa wa kijinsia na kuleta mabadiliko chanya kwa wanawake. Duniani kote, makampuni na watu binafsi huadhimisha siku hii kwa kusherehekea mafanikio ya wanawake huku wakitoa elimu dhidi ya ubaguzi wa kijinsia, na kwa kufanya hivyo, huvunja ubaguaji na kuchangia katika juhudi zinazolenga kujenga ulimwengu wenye usawa. 

Kama jukwaa la wanachama linalojumuisha Wakurugenzi Wakuu kutoka zaidi ya kampuni 160, sekta mbalimbali nchini Tanzania, CEOrt kwa muda mrefu imekuwa mtetezi mkubwa wa utofauti na ushirikishwaji. Uwakilishi wa wanawake katika uanachama umeendelea kukua kwa kiasi kikubwa ndani ya miaka mitatu iliyopita, na ongezeko la 86% kwa viongozi wa kike ndani ya CEOrt. Vilevile, CEOrt imedhamiria na kuweka malengo dhabiti kwa mpango wake wa uongozi bora, CEO Apprenticeship Programme, unaotazamia kuongeza ushiriki wa wanawake kutoka 25% hadi 40% ifikapo mwaka wa 2025.

CEOrt ina furaha kumkaribisha Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akiwa mzungumzaji mkuu na Mgeni Rasmi. Balozi Mulamula atamuwakilisha Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye CEOrt inampongeza kwa mafanikio yake katika nafasi ya ujumuishaji wa jinsia. Kupitia Rais Samia, viongozi wa sekta binafsi wanatambua ari na ushirikiano wa uongozi katika kuboresha mazingira ya biashara, kuwezesha Uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni kuelekea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya taifa. Vilevile, Raisi Samia ameonyesha mtazamo shirikishi wa uongozi, ambao unadhihirika katika ongezeko la uwakilishi wa wanawake katika nafasi za uongozi serikalini kwa athari endelevu katika ukuaji wa uchumi wa nchi katika miaka ijayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa CEOrt, Santina Majengo-Benson, amesisitiza dhamira ya shirika kutetea hadharani usawa wa kijinsia na utofauti. "Kuwa na wanawake katika nafasi za uongozi ni muhimu sana. Kwa mtazamo wa kibiashara, ongezeko la uwakilishi wa wanawake katika nyadhifa za uongozi hupelekea kuimarisha utendaji kazi - baadhi ya tafiti zimeonyesha; kuwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kike husababisha ongezeko la asilimia tano la thamani ya soko la shirika," alisema. CEOrt ina nia ya kutumia ushawishi wao wa uongozi ili kukuza usawa wa kijinsia kwa kusaidia uwezeshaji wa wanawake, wanawake walio katika uongozi na kuhamasisha mwonekano chanya wa wanawake wote. Ndivyo tutakavyovunja upendeleo kwa kweli.Kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani 2022 ni Vunja Upendeleo, ambayo inahimiza ulimwengu kukomesha dhana potofu za kijinsia katika jamii, mahali pa kazi, mashuleni, na vyuoni, katika siku hii na siku zijazo. Katika kuadhimisha siku hii na dhima, wanachama na mzungumzaji mkuu, kutoa wito kwa washiriki 'kufikiri usawa na kuongoza kwa busara'.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...