Kampuni ya Afrieuro Digital Ventures imesema imefanya marekebisho katika usajili wa mtandao kwa wafanyabiashara wanaouza bidhaa zao kupitia Zoom na Kupatana ili kuziba mianya kwa wale wasio waaminifu.

Kuanzia sasa wafanyabishara wanaojisajili katika kampuni hiyo kwa ajili ya kutangaza bidhaa zao, wataruhusiwa kujisajili si zaidi ya mara tatu ili kudhibiti wizi wa mitandaoni.

Hayo yamesemwa na Meneja Mkuu wa Afrieuro Digital Ventures, Makusaro Tesha wakati akielezea kuhusu kuungana kwa mitandao hiyo ‘Kupatana.com’ na ‘Zoomtanzania.com’ ili kutoa huduma zake kwa urahisi, haraka na salama zaidi kwa wanunuzi na wauzaji mtandaoni.

“Ukiangalia mwanzo kupatana au zoom ilikuwa unafanya usajili na kisha unaanza kutumia moja kwa moja lakini sasa hivi mambo yatabadilika, hautakuwa unajisajili kwa barua pepe kwa sababu hata tukimfungia mtu leo, ataenda ataweka email nyingine utarudi tena,” alisema.

Tesha alisema kwa sasa ili mtu aweze kujisajili katika mitandao hiyo, itamlazimu kutumia nambari zake za simu alizosajilia laini na mwisho kujisajili itakuwa ni mara tatu pekee.

“Sheria ya nchi huwezi kumilikki namba zaidi ya tatu kama utagundulika kwamba unashiriki katika utapeli tutakufungua akaunti yako ya kwanza, ukiridia ya pili na ukifungiwa zote tatu hutaweza tena kujisajili unakua nje ya mfumo,” alisema.

Tesha alisema Zoom na Kupatana wanashirikiana na vyombo vya sheria katika kutoa msaada kwa yule ambaye ametapeliwa pia wamekuwa wkaiwashauri wateja kujilinda kuhakikisha hawatumi fedha kabla ya kupokea mzigo.

“Haiwezekani mtu akakwambia ninauza hiki kifaa 250,000 nitumie hela nikutumie hapana lazima ufike sehemu ambayo ni salama ukague mzigo na kisha umlipe na sisi kama watangazaji hatuhusiani na fedha za mteja au anayetangaza,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Afrieuro Digital Ventures, Sammy Ben Abla alisema kampuni mbili kubwa za mtandao ambazo huko nyuma zilikuwa na ushindani mkubwa kwenye mitandao, Zoom na Kupatana zimeungana na kuwa chini ya kampuni moja ya Afrieuro Digital Ventures ambayo ndiyo imepata haki zote za kumiliki tovuti hizo zote mbili na kuongeza wigo mpana nchini Tanzania.

Alisema hiyo ni fursa nzuri zaidi kwa watumiaji wa mitandao kuweza kujipatia bidhaa mbalimbali kupitia tovuti hiyo.

“Hii ni fursa nzuri kwetu, lakini haswa kwa watumiaji wa mitandao walio Tanzania kwa kuwa tutaweza kukuza na kuboresha zaidi uwepo wa uhakika wa soko la mtandaoni na kutoa fursa zaidi za mauzo na matumizi rahisi ya mifumo hii kwa watumiaji wa ina zote," alisema.

Abla alisema kwa sababu ya kiwango cha juu cha uhamasishaji na ufahamuwa mifumo hiyo miwili nchini Tanzania na uzoefu wawatumiaji wa simu za mkononi, Kupatana.com itabaki kuwakama jina la chapa huko mbeleni lakini kwa sasa tovuti zotembili zitaendelea kutumika kama zilivyo.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...