Na Mwandishi Wetu- Dodoma
Katika mazingira ya kawaida mapokeo ya watu na kila mtu ana mapokeo yake na wanajiuliza kwa nini katiba imewekwa mwisho
Hayo yamezungumzwa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Geophrey pinda wakati akizindua magari mawili ya Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora katika ofisi Za Tume hiyo zilizopo Kilimani Jijini Dodoma.
" Nchi Sasa tuko kwenye maendekeo na wakati mwingine unaangalia katiba ndiyo lakini je nini adhari yake kwenda kwenye swala la utoaji haki." amesema Pinda
Pinda amesema Katiba Ina haki zote wale wanaokwenda kuisimamia labda ndo Wana matatizo tatizo
"Katiba hii ni kama Bibilia kila mtu akinyanyuka na kuona mwenzake alivyotafsiri Biblia ni tofauti naye anasema ngoja na mimi nisimame niwe mtafsiri dini ni nyingi lakini hakuna aliyebadili mstari hata mmoja katika kitabu hicho." - Pinda
Aidha Pinda amesema hiyo ni demokrasia na haiwezekani kuwaweka watumishi wa Mungu pamoja katika hatua ya kubishana kwenye kitabu Kitakatifu, hivyo hata katiba iliyopo ndiyo Mana Rais amesema hilo swala lipewe muda na kuangalia ni namna gani watafanya marekebisho.
Hao walioianzisha na waliokuja na mjadala wote hao ilikuwa ni katika kuimarisha upatikanaji wa haki maeneo mbalimbali.
"Umuhimu wa Katiba mpya na umuhimu wa Katiba iliyopo hivi ndivyo Rais Samia anavyotekeleza kwa katiba hii jinsi ambavyo wananchi watakavyofikiwa na haki." amesema Naibu Waziri Pinda
Hata hivyo Pinda amesema Rais Samia anastahili pongezi kwa kuliona hilo. Lakini kwa watu wengine kubishana kwa ajili ya Katiba huwezi kuzuia kwa sababu kila mtu anaangalia jinsi alivyosoma na kuelewa mistari hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora Mathew Mwaimu (JajiMstaafu) ameishukuru Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia kwa kuipatia Tume hiyo fedha na kuwezesha kununua magari hayo
"Kwetu sisi Watumishi wa Tume tunaona kuwa hii ni ishara tosha kwamba Serikali inajali na kuona umuhimu wa kuiwezesha tume kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa kuwa swala la kukuza na kuimarisha haki za binadamu na misingi ya utawala bora ni nguzo muhimu ya kuboresha maisha ya wananchi." - amesema Mwenyekiti Jaji Mstaafu Mwaimu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...