Na Mwandishi Wetu, Serengeti, Mara.
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Ridhiwani Kikwete (MB) ametoa salamu za pongezi za kutimiza mwaka mmoja wa Urais, Kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, huku akimpobgeza kwa kufanikisha upimaji wa eneo la kilometa (KM) 83, za mpaka huo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mhe. Ridhiwani Kikwete ametoa pongezi hizo mapema leo Machi 19, 2022 akiwa 'field' katika eneo la Hifadhi ya Serengeti kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya akiwa ameambatana na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.
"Hongera sana Mhe. Rais kwa kutimiza mwaka mmoja wa uongozi wako. Kwa hakika Watanzania tunajivunia sana, hapa tulipo ni eneo la Hifadhi ya Serengeti nikiwa pamoja na Kamati ya Bunge inayosimamia masuala ya Ardhi, Maliasili na Utalii"
"Furaha yetu ni kwamba leo tumesimama hapa katika mpaka unaogawa nchi ya Tanzania na nchi ya Kenya.
"Mpaka huu huwa ni kilio kikubwa sana hasa katika eneo la utalii.
Kwa miaka takribani mitatu, tumekuwa na kilio cha kutafuta ambao una KM zisizopungua 60 ili uweze kuhifadhi lakini pia uweze kutupatia kipato na sifa ile ambayo mbuga yetu ya Serengeti iliyokuwa nayo." Alisema Mhe. Ridhiwani Kikwete.
Aidha, amemshukuru katika kufanikisha upimaji huo ambao kwa sasa ni matunda kwa Nchi.
"Katika kipindi chako cha mwaka mmoja, Mhe Rais, umefanikisha upimaji wa eneo la KM83, KM 23 zaidi ya zile ambazo zilikuwa zimeahidiwa mwanzo, sisi kwa niaba ya wizara tunaendelea kukupongeza na kukushukuru kwa jinsi ambavyo umekuwa unatupa ushirikiano mkubwa sana,
"Kwa kweli tunakupongeza sana kwa mafanikio makubwa haya ambayo unayapata.. Mhe Rais tunaendelea tena kukupongeza na kutakia afya njema na Mwenyezi Mungu akujalie sana katika safari yako ya uongozi wa Nchi yetu." alimalizia Mhe. Ridhiwani Kikwete katika salamu hizo za mwaka mmoja wa Rais Madarakani.
Kamati hiyo pia ilitembelea maeneo mbalimbali ya mpaka huo ikiwemo eneo hilo la Uwandani kwa ajili ya kukagua kazi iliyokwisha fanywa na Wizara hiyo ya Ardhi ya kuimarisha mpaka kati ya Kenya na Tanzania, ambapo Serikali ilitenga Bilioni 5.7.
Mwaka mmoja wa Rais Samia iliyopewa alama ya utambulisho wa #Samia365 umekuwa na mafanikio makubwa ambapo katika kipindi chote miradi mbalimbali iliyoanza na mipya imekuwa ikitengewa fedha na kufanikishwa huku ile ya awali ikiendelezwa katika falsa ya Kazi iendelee.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...