Na Janeth Raphael -Dodoma

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amepitishwa na Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara leo Machi 31, 2022 nafasi iliyokua inashikiliwa na Mzee Philip Mangula ambaye kwa ridhaa yake ameomba kujiuzuru nafasi hiyo.

Akitoa taarifa ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichokaa leo Jijini Dodoma Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka amesema kwa kauli moja kikao hicho kimempendekeza na kumpitisha kugombea nafasi hiyo ambapo kesho atapigiwa kura na wajumbe baada ya aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula leo Alhamisi  Machi 31, 2022 kuwasilisha barua ya kujiuzuru kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM barua iliyokelewa na mwenyekiti wa chama yenye lengo la kuachia nafasi hiyo kwa utashi wake mwenyewe.

Katika hatua nyingine Ndg shaka amesema Chama cha Mapinduzi kimewarudishia Kadi zao za Uanachama waliokua wanachama na kuhamia vyama vingine Benard Membe na Abdalah Diwani baada ya kamati Kuu ya CCM kujiridhisha na maombi yao yakuomba kurudishwa CCM.

Mapema leo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan, amekagua  maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya  Kikwete, utakao fanyika kesho April 01, 2022.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...