Na Jane Edward, Arusha

Baadhi ya Mikoa ya Kagera, Bukoba, Dodoma na Ya Kanda ya kaskazini inatajwa kuwa kinara katika matumizi ya maharage aina ya Jesca kwaajili ya kuboresha tendo la Ndoa.

Sababu kubwa inayotajwa ni kutokana na maharaje hayo kuwa na kiwango kikubwa cha madini ya Zinki yaliyo mhimili mkubwa kwenye kurutubisha nguvu za kiume.

Akizungumza na waandishi wa Habari na Watafiti, Shida Nestory Mahenge wakati wa ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) amesema maharage hayo ni moja kati ya maharage yanayopendwa kutokana na ubora uliopo.

Amefafanua kuwa maharage pia yanaweza kusagwa yakawa unga na kupikiwa uji ambao ndiyo hupelekea mtumiaji kupata nguvu ya kutumikia familia pamoja na kukuza kiwango cha vitamini kwenye mwili wake.

"Yaani ubora wa huu unga wa maharage ya Jesca umetokea kupendwa wananchi badala ya kutoka kazini na kwenda kunywa bia, sasa ni wakati wa kutumia uji wa Jesca kwàajili ya afya zaidi" Alisema

Kwa upande wake Daktari wa binadamu Bunini Manyilizu amesema kwenye maharage mengi kuna protini lakini utofauti uliopo kwenye Zinki inasaidia kuamsha hisia za Mwanaume.

Amefafanua kuwa pamoja na kwamba mwanaume anapaswa kutokuwa mvivu wakati wa tendo lakini uwepo wa maharage ya Jesca yanaonekana kupendwa na na kutumiwa na watu wengi hali inayoashiria kuna ukweli ndani yake.

Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI Seliani kinatajwa kuwa ndio kimegundua uwepo wa maharage ya Jesca na kufanya Utafiti na kugundua ufanyaji wa kazi zake katika mwili wa binadamu.

Mtafiti Shida Nestory Mahenge akifafanua kuhusu maharage ya Jesca na umuhimu wake.
Pichani bidhaa za nafaka zikiwa mezani.
Mtafiti akionyesha unga wa maharage ya Jesca na maharage yenyewe kwa waandishi wa habari na Watafiti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...