Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka Wazanzibari kuendelea kuwa wamoja ili kuifikia Zanzibar yenye Neema.

Mhe. Hemed ametoa kauli hiyo wakati akiwasalimia Waumini wa Mskiti wa Mwembetanga alipojumuika nao katika Ibada ya Sala ya Ijumaa.

Amesema umoja uliokuwepo Zanzibar ni wa kudumishwa hivyo ni vyema kuendeleza na kuwarithisha kizazi kijacho kiweze kufikia malengo ya kuwa na Jamii yenye uelewa na yenye umoja na mshikamano.

Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ametumia fursa hiyo kukemea tabia ya wachache wanaopotosha Jamii kwa kueneza fitna na kuwagawa Wazanzibari jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya Zanzibar.

Sambamba na hayo Mhe. Hemed ameeleza kuwa Viongozi wa Serikali ya Awamu ya Nane wataendelea kujumuika na wananchi katika matukio mbali mbali ya kijamii jambo ambalo linawaweka karibu na wananchi wanaowaongoza na kuweza kufikisha kwa urahisi Changamoto zinazowakabili.

Pamoja na hayo Mhe. Hemed amewasihi Waislamu kuhurumiana hasa katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kupata Radhi za Allah Mtukufu.

Akitoa hutuba katika Sala hiyo Ustadh Ramadhan Saleh amewataka waumini hao kutumia vyema Neema walizopewa hasa Neema ya kuwepo kwa mitandao na kueleza kuwa jambo hilo litasaidia kuwafikisha kwenye uchamungu na kuwanasihi kuacha kutumia katika yale asiyoyaridhi Allah.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akitoa salamu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kukamilisha Ibara ya Sala ya Ijumaa katika Msikiti Mwembetanga Wilaya ya Mjini.



Waumini wa Dini ya Kiislamu wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati akisalimiana nao baada ya Sala ya Ijumaa.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...