Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amesema serikali inatarajia kuanza ujenzi wa stendi ya kisasa katika manispaa ya Bukoba kwa kupeleka awamu ya kwanza shilingi bilioni moja kwa mwaka wa fedha 2022/23 nakuelekeza Manispaa ya Bukoba nayo kutenga bajeti kwa ajili ya kutekeleza mradi huo muhimu.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kagera katika uwanja wa Mashujaa wa Mayunga uliopo Bukoba. Amesema kwa kutambua umuhimu wa mradi huo pamoja na ule wa ujenzi wa soko tayari serikali imejipanga katika kushughulikia changamoto hizo kikamilifu.

Aidha Makamu wa Rais amesema Serikali inaendelea kujenga na kuimarisha miundombinu ya usafirishaji ikiwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa meli ya MV Mwanza (Hapa Kazi Tu), kwa manufaa ya wananchi wa Bukoba na kanda yote ya ziwa, ujenzi wa Meli hiyo unatarajiwa kukamilika Septemba 2022.

Halikadhalika amewataka wananchi wa Mkoa wa Kagera kuendelea kulinda amani na umoja pamoja na kujitokeza katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Mwezi Agosti mwaka huu.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Charles Mbuge ameishukuru Serikali kwa kuupa kipaumbele mkoa huo ambapo mpaka kufikia mwezi Februari mwaka 2022 tayari serikali imepelekea kiasi cha shilingi bilioni 315 kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu, miundombinu, afya na kilimo.
Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na Viongozi na wananchi wa Mkoa wa Kagera katika Uwanja wa Mashujaa wa Mayunga uliopo Bukoba mkoani Kagera leo tarehe 18 Machi 2022.Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwaaga wananchi waliojitokeza kumsikiliza katika Uwanja wa Mashujaa wa Mayunga uliopo Bukoba mkoani Kagera leo tarehe 18 Machi 2022.Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipanda mti katika Uwanja wa Mashujaa wa Mayunga uliopo Bukoba mkoani Kagera wakati alipofika kuzungumza na wananchi pamoja na viongozi wa Mkoa huo leo tarehe 18 Machi 2022

Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwasili katika uwanja wa Mashujaa wa Mayunga uliopo Bukoba mkoani Kagera kwaajili ya kuzungumza na viongozi na wananchi wa mkoa huo leo tarehe 18 Machi 2022.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...