Mradi wa mafunzo ya kidigitali unaofahamika kama TECH4ALL DigiTruck wa unaodhaminiwa na kampuni ya Huawei nchini Kenya umetambuliwa kimataifa kwa kuongeza idadi ya wanawake wanaofuata kozi za teknolojia na kufanya kazi katika sekta ya ICT.

Mpango huo unaoendeshwa na Kampuni ya Huawei kwa ushirikiano na Safaricom, Wizara ya TEHAMA ya Kenya, Kompyuta kwa Shule za Kenya, na shirika lisilo la kiserikali la kimataifa la Close the Gap ambayo pia yalitambuliwa kwa michango yao katika kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs).

Mradi wa DigiTruck ulizinduliwa nchini Kenya kwa mara ya kwanza mwaka wa 2019. Mradi huo unalenga kuleta teknolojia ya kidijitali katika mikoa yenye hali duni ya rasilimali na kuwawezesha watu kupata elimu bora na kuboresha maisha yao. Kufikia mwisho wa 2020, mradi umetoa huduma kwa maeneo 13 ya vijijini nchini Kenya, wanafunzi na walimu 1300, walitumia hadi saa 22,000 kwa mafunzo.

DigiTruck ni darasa tembezi (Mobile Class) lililobadilishwa kutoka kwa kontena la lori lenye ufikiaji wa mtandao wa wireless, ambapo wanafunzi wanaweza kujifunza ujuzi wa kidijitali na kupata huduma ya intaneti.

"Ushindi huu ni utambuzi wa hali ya juu wa juhudi zetu pamoja na Huawei na washirika wengine katika kuunganisha wateja wetu kidijitali," alisema Peter Ndegwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Safaricom.

DigiTruck ni sehemu ya mpango wa ujumuishi wa kidijitali wa Huawei TECH4ALL, unaolenga kutumia teknolojia, programu na ujuzi ili kuwawezesha watu na mashirika. Katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, TECH4ALL pia inaendeshwa nchini Afrika Kusini, Ghana na Mauritius.

Nchini Afrika Kusini, TECH4ALL imenufaisha zaidi ya wanafunzi 52000 kutoka zaidi ya shule 90 za msingi mijini na vijijini; nchini Mauritius, mradi unatumia kamera za chini ya maji kufuatilia miamba ya matumbawe inayotishiwa kwa wakati halisi ili kulinda na kurejesha hekta 5 za mfumo ikolojia wa miamba hiyo wakati nchini Ghana, mradi unalenga kuunda maudhui ya kidijitali kwa walimu na wanafunzi wa ndani.

“Nimefurahi kuona kwamba UNESCO na Huawei zinafanya kazi na taasisi zetu za kitaifa, hasa zile zilizopewa mamlaka na Serikali ya Ghana kukuza ujumuishaji kamili wa TEHAMA katika mfumo wa elimu,” alisema Yaw Osei Adutum, Waziri wa Elimu.

"Teknolojia ya habari na mawasiliano ICT inaweza kusaidia kuharakisha maendeleo kuelekea kila Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, hasa SDGs muhimu ikiwa ni pamoja na Elimu Bora, Usawa wa Jinsia na Mabadiliko ya Tabianchi. Kama kampuni ya kimataifa ya TEHAMA inayofanya kazi katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, tunajaribu kufungua uwezo wetu wa TEHAMA pamoja na washirika wa ndani na wa kimataifa kwa ajili ya maisha bora, jamii bora, mazingira bora na mustakabali bora wa watu na vizazi vijavyo kutoka kanda hii "alisema Bw. Yang Chen, Makamu wa Rais, Huawei Kanda ya Kusini mwa Afrika.






DigiTruck, darasa linalotembea ambalo hutoa mafunzo ya ujuzi wa kidijitali kwa wanajamii.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...