Na Jane Edward, Arusha

Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 61 ya ardhi tunayoishi iko hatarini kuwa jangwa kutoka na kilimo kisichozingatia kanuni bora za kilimo kwa kutumia kemikali nyingi hali inayosababisha ardhi kuchoka, mimea mingine isikuwe na ufugaji holela.

Hayo yamebainishwa na meneja miradi Island of Peace (IDP)Ayesiga Hiza wakati wa ufunguzi rasmi wa Mradi mpya wa Kilimo Endelevu uliofadhiliwa na serikali ya ubelgiji Mkoani Arusha kwa lengo la kuangalia upungufu wa chakula katika kaya .

Aidha amesema kuwa mradi huo ni wa miaka mitano ambapo unalenga kuinua mifumo Endelevu ya chakula na kumuangalia mkulima katika usindikaji wa chakula na kuangalia masoko yanavyo kwenda.

"Ardhi ni kitu muhimu sana ambacho kila mtu anakihitaji kwenye ardhi,kuishi kwenye ardhi,kula kwenye ardhi pamoja na shughuli za kilimo lakini tunaitunzaje hii ardhi ili iweze kutusaidia sisi na vizazi vijavyo" Alisema Ayesiga

Amefafanua kuwa mradi huo unatekelezwa katika wilaya ya Arusha, Arusha jiji na kwamba chakula kinacholiwa Arusha kinatoka katika maeneo yaliyoizunguka Arusha na ndipo wakulima wengi wapo.

"Tukiweza kuboresha mfumo Endelevu wa chakula na wakulima hao wakaweza kulima chakula kwa usafi na usahihi ambapo swala la chakula na usafi linazingatiwa sana katika mradi huo" Alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa IDP Ludovic Jolly amesema kuwa mabadiliko ya tabia nchi ndiyo yanasababisha kuwepo kwa changamoto kwenye upatikanaji wa chakula bora ambapo kilimo endelevu kitashirikiana na serikali katika kupunguza adha hiyo.

Ameongeza kuwa karibia theluthi moja ya wilaya hapa nchini zinaripoti uhaba wa chakula ambapo kuna ya kuboresha mifumo ya chakula ambapo theluthi moja za wilaya hapa nchini zinaripoti uhaba wa chakula na kwamba kilimo endelevu kinatumia mfumo wa ekoloji ili kuboresha mifumo ya kilimo na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

"Kilimo endelevu kitashirikiana na wadau mbalimbali wa serikali katika kuboresha kilimo endelevu sanjari na kupata wawakilishi wa kuwatumia katika mradi huo endelevu.

Naye Kaimu Mkuu wa Mkoa Arusha Richard Ruyango amesema kuwa serikali ina imani kuwa wanufaika wa Mradi huo utakuwa ni wa wananchi wote wa Tanzania kwa kuwa mradi huo utatekelezwa hapa nchini.

Amefafanua kuwa utekelezaji wa mradi huo wa Kilimo Endelevu utasaidia Watanzania kupata ajira kutokana na shughuli zitakazo kuwa zinafanyika na Serikali itatoa ushirikiano wa kutosha na kama Mkoa hawata kuwa kikwazo cha kukwamisha kwa mradi huo.

Ludovic Jolly Mkurugenzi IDP akipokea kitabu cha maelekezo ya Mradi kilimo endelevu kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha Richard Ruyango.

Ayesiga Hiza akiongoza zoezi la kukata utepe uliofanywa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha Richard Ruyango .

Kaimu Katibu tawala Mkoa Arusha Chitukulo Akizungumza na washiriki wa mkutano huo.

Wadau wa kilimo




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...