Na Mary Margwe, Simanjiro
MANGARIBA wa jamii ya Kimasai wapato 20 jana wamesalimisha dhana zao za kazi maarufu kama shoka ( Omorunya) kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Carolina Mthapula zilizokua zilkitumika kwa ajili ya kukeketea watoto wa kike wa jamii yao mbele ya maelfu ya watuwaliohudhuria siku ya maadhimisho ya wanawake duniani.

Mwenyekiti wa Mangariba hao Naserian Alais kutoka kijiji Lobosoiti A Kata ya Emboret wilayani Simanjiro mkoani Manyara alisema wao walikua na kikundi chao maarufu kwa jina la Napokie chenye watu wapatao 20 waliokua wakijihusisha na vitendo kwa ukatili kwa kuwakeketa watoto wa kike.

Alais alisema kuacha kuendelea na vitendo hivyo vilitokana na kukalishwa chini na Mkurugenzi wa shirika la Ushirikishwaji na Uwezeshaji wa Kijinsia ( FPCT ) Elia Ngurumwa na timu yake kuanza kulivalia njuga suala hilo kisha ndipo wakaanza kuwaelimisha juu ya kuachana kabisa na hizo mila potofu za ukatili dhidi ya watoto wa kike.

" Tunaishukuru sana serikali pamoja na hilo shirika la FPCT kwa kuwa nasi katika kutuelimisha juu ya kuacha kabisa hii mila ya kuwakeketa watoto wetu, na kweli tumefanikisha chini ya Mkurugenzi wa shirika hili Elia Ngurumwa pamoja na time nzima, hakika wamefanya kazi nzuri sana kwetu, na leo hatimaye tumekabidhi vifaa vyetu ili kuachana kabisa " alisema Alais.

Aidha alisema ni vizuri kuwapa watoto wa kike haki zao za msingi kwa kuiwasomesha kitokufanya hivyo ni kuwanyanyasa watoto wa kike na kuwanyanyasa watoto wasio na hatia, ambapo walikua wakifanyiwa ukatili huo kuanzia mtoto alipokua na umri wa mwaka mmoja hadi 18.

Aidha alifafanua kuwa ukeketaji umeleta madhala makubwa Kwa watoto wa kike, Kwa maana akipata mimba na kwenda kujifungua hutokwa na damu nyingi na pengine baadaye hupoteza maisha kabisa.

" Ndio maana tumekaa tumetafakafna sasa tumeamua kuwakeketa watoto wetu wa kike, na ikumbukwa kuwa ndio maana sasa tumesimama na kuelimisha kwamba tumekataa kabisa ukeketaji Kwa watoto kwa watoto wetu, sasa tumeona madhara yake, naawaambia wanawake wote wa kimasai tusimame imara kulipinga hili hatutaki tena kuwakeketa watoto wetu ,tumeona kufanya hivyo ni kutafuta laana maana tunakua tumewafanyia ukatili mkubwa, kikubwa na cha msingi ni kuwapatia elimu" aliongeza Ngariba huyo.

Kufuatia hill Katibu Tawala wa Mkoa huo Carolina Mthapula alimpongeza mama huyo kwa kitendo tendo walichokitenda cha kukabidhi vifaa kwake kuwa ni kitendo cha ujasiri na pia ni upendo katika jamii, maana wamethubutu wenyewe baada ya kuelimishwa, na hivyo ameitaka halmashauri ya wilaya hiyo kuhakikisha wanashauriwa kuunda kikundi ili waweze kupatiwa fedha za kuanzisha biashara ili kujikwamua kiuchumi.

Hata hivyo katibu Tawala huyo, aliwataka hao Mangariba kuhakikisha sasa wanawekeza nguvu zao katika kuwasomesha watoto wa kike na wakiume badala ya awali walipokua wakielekeza nguvu nyingine katika kuwaza juu ya ukeketaji wa watoto wa kike, hivyo sasa waone Kama vilishapita wafungue ukurasa mpya wa kuwainua watoto kimasomo na kufuafilia maendeleo yao mashuleni.

Naye Mkurugenzi wa shirika la Ushirikishwaji na Uwezeshaji wa Kijinsia ( FPCT Maasai Gender Particition and Empowerment Project Simanjiro) Elia Ngurumwa alisema kikundi hiko kwa sasa tayari wamekubaliana na mabadiliko ya maendeleo, kwani baada kuwasaidia kuwaelimisha na kuelewa waliweza kwenda kwenye ofisi ya kijiji cha Lobosoiti A na kuwaelezea viongozi kuwa kazimya kukeketa sasa wameiacha kabisa.

Hata hivyo Ngurumwa aliongeza kuwa baada ya hapo walikua wakitembea kila kitongoji kujielezea hilo, kisha kwenda kwenye mikutano ya wanawake na kujielezea kuhusiana na kuachana na hizo mila potofu ya kukeketa watoto wa kike.

" Shirika hili limeanzishwa miaka miwili iliyopiga ikiwa na dhana muhimu za usawa wa jinsia ndani ya jamii, ikiwa na lengo la kupunguza migogoro isiyo ya lazima, haki ya kufikia, kuitumia kunufaika, na kumiliki rasilimali ya nchi, haki ya kufikia na kufaidi huduma za msingi" alisema Ngurumwa.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Carolina Mthapula akionyesha dhana au kifaa kinachotumika kwenye shughuli ya ukeketaji wa watoto wa kike maarufu kama shoka ( Omorunya ) aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa kikundi hiko cha Mangariba Naserian Alais (kulia ) kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo Dk. Suleiman Serera ambapo Mangariba hao wamekua wakiish katika Kjiiji Lobosoiti A Kata ya Emboret wilayani Simanjiro mkoani Manyara alisema wao walikua na kikundi chao maarufu kwa jina la Napokie chenye watu wapatao 20 waliokua wakijihusisha na vitendo kwa ukatili kwa kuwakeketa watoto wa kike ambao Kwa sasa wameacha kabisa kujihusisha na vitendo hivyo, Picha na Mary Margwe
Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Carolina Mthapula akiwapongeza baadhi ya Mangariba kati ya 20, mara baada ya kukabidhi vifaa vyao kwake jana kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani iliyofanyika kimkoanwilayani Simanjiro, ambapo mgeni rasmi aliwa Katibu Tawala huyo, kulia ni mkuu wa Wilaya hiyo Dk.Suleiman Serera, Picha na Mary Margwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...