Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima leo Jumatano Machi 16, ametembelea eneo la ajali iliyotokea jana usiku wilayani Handeni na kuua watu wanne.

Akiwa katika eneo la ajali, RC Malima amezungumza na baadhi ya watu walioshuhudia ajali hiyo.

Baadhi ya mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo, wamemueleza RC Malima kuwa ilitokea baada ya gari aina ya Costa iliyokuwa na abiria ikitokea Korogwe kuelekea Handeni kugonga baadhi ya wananchi waliokuwa wakisaidia kuziba pancha kwenye hiace iliyokuwa imepaki pembeni ya barabara.

"Hiace ilikuwa 'imeburst' kulikuwa na wanakijiji wanasaidia kubadilisha tairi, wakati costa inakuja akawa anaelekezwa asimame lakini kwa sababu haikuwa na taa ikagonga wale wanakijiji waliokuwa wanasaidia na kuanguka huko bondeni, kwa hiyo waliopata ajali wengi ni wananchi," amesema shuhuda huyo.

RC aliongozana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Safia Jongo. Majeruhi wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni wakiendelea na matibabu.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...