Na Jane Edward, Arusha

Utafiti mdogo uliofanywa kwa jamii ya wafugaji wa asili wanaoishi katika vijiji vitano vya wilaya ya Simanjiro Mkoa Manyara kuhusu uwezo wa jamii hiyo kukabiliana na majanga yakiwemo yanayotokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi umebaini kuwepo kwa njia nyingi za asili zenye kuleta matokea chanya kwa jamii hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha katika uzinduzi wa  ripoti ya kukabiliana na majanga ya asili Wilayani Simanjiro, Afisa mifugo na uvuvi Dkt Swakeh Masaza amesema kwa sasa jamii ya kifugaji inakabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi.

Aidha ripoti ya matokeo ya utafiti huo uliofanywa na shirika la Pingo's Forum kwa ufadhili wa shirika la kimataifa la masuala ya maendeleo (OSIEA)ambapo imezinduliwa jijini Arusha huku njia moja wapo ya asili  ikiwa ni ya wafugaji wa asili kuhama kwa ajili ya kuisalimisha mifugo

Ameongezea kuwa kwa sasa wafugaji wameanza kujikita kwenye kilimo na kuhama hama ili kutafuta sehemu yenye maji ya uhakika na malisho ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.

Gideon Sanago ni afisa mabadiliko ya tabia nchi Pingo's ambapo anasema jamii ya wafugaji hutumia utabiri wa asili ili kung'amua baadhi ya mambo lakini kwa sasa elimu hiyo ya maarifa ya  asili inapotea kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

"Uwepo wa wafugaji kuwa na tabia ya kuhama hama unasaidia kuacha nafasi ya hiyo sehemu hiyo  kustawi na kutunza mazingira na inasaidia mfumo wa mazingira na ustawi kuendelea kustawi vizuri zaidi" Alisema

Amesema kuwa maeneo mengi yenye wafugaji wa asili yanatunzwa tofauti na wengine na kwamba ripoti hiyo ni kwaajili ya watunga Sera ili kuwezesha wao kuelewa na ikiwa tayari itaandikwa kwa lugha rahisi.

Kwa upande wake afisa jinsia kutoka Pingo's Forum Nailejileji tipap anasema ripoti hiyo itasaidia kupata taarifa ya kuitumia kila siku na kutoka nje zaidi ya Sayansi ambayo itatusaidia kupata maarifa mengine na kuyatumia kila siku.

Hata hivyo ripoti hiyo imefanyika toka mwaka jana na eneo la simanjiro katika vijiji vitano limechaguliwa kwa lengo la kuangalia namna wafugaji wa asili wanavyokabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo mabadiliko hayo yamesababishwa na shughuli za kibinadamu zinazomsaidia meanadamu kujipatia kipato.

Aidha ili kuhakikisha kuwa njia hizo za asili zinaboreka na kuwa endelevu wataalamu wa sheria na mabadiliko ya tabia nchi wanashauri kuwepo kwa sera rafiki zinazomtambua mfugaji wa asili.

 Wadau wa mabadiliko ya tabia nchi Wakishika ripoti ya kukabiliana na majanga ya asili kuashiria uzinduzi wa ripoti hiyo .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...