Na Khadija Kalili,Kibaha

Imamu Mkuu  na Mwenyekiti wa Shirika la Dawate Islami Tanzania An Initiative of Dawate Islami for  the Welfare and Aid of the People in need (FORF) Maulana Ahmed  Raza Qadri Attari ameongoza zoezi la kugawa futari kwa Waumini wa dini ya Kiislamu zaidi ya 300 katika kaya za watu wasiojiweza Wilayani Kibaha Mkoani Pwani .

Zoezi hilo ambalo lilifanyika katika maeneo ya Mikongeni , Kipangege, Sofu na  Kibwemwenda Msese ambapo ni mpakani mwa Kibaha na Kisarawe .

Akizungumza na Waandishi wa Habari Maulana Ahmed Raza Qadri alisema msaada waliotoa ni futari pamoja na daku huku akiwatakia waumini hao  swaumu njema.

Maulana Ahmed Raza aliongozana na jopo la Mashaikh na Maulana wengine ndani ya Taasisi hiyo ya FORF.

"Kabla ya kugawa msaada huu tulipita kuwakagua na Hawa aliopata futari hii Kamati iliridhika kuwa wamekidhi vigezo ambapo Kila kaya wamepatiwa sukari, Tambi, mafuta ya kupikia, mchele, maharagwe,chumvi na  majani ya chai ambavyo vitawasaidia kwa ajili ya futari na daku "alisema Maulana Ahmed Raza Qadri Attari.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...