Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

KATIKA Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mteja Duniani Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA)imeanzisha mpango maalumu wa kutatua changamoto za huduma za mawasiliano nchini, kwa kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta hiyo.

Utaratibu wa TCRA ni kutaka kuboresha huduma za mawasiliano pamoja na kutatua changamoto kati ya watoa huduma na mdhibiti hii itafanya sekta ya mawasiliano kukua zaidi.

wadau waliowakutanisha ni watumiaji na watoa huduma za mawasiliano Kama kampuni za simu,Ving'amuzi na watoa huduma wa redio na luninga.

Akizungumza Dar es Salaam Jana, katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta Mawasiliano,Mkurugenzi wa Leseni na Ufuatiliaji TCRA, John Daffa,alisema wadau waliowakutanisha ni watumiaji na watoa huduma za mawasiliano Kama kampuni za simu,Ving'amuzi na watoa huduma wa redio na luninga.

Alisema tangu kuanzishwa kwa Mamlaka hiyo hawajawahi kuwakutanisha watendaji hao na wananchi kwa ajili ya kujadili, kutatua na kusikiliza changamoto za huduma za mawasiliano ana kwa ana.

Daffa alisema kuwakutanisha wadau hao ni sehemu ya Maadhimisho ya siku ya haki ya haki ya mteja ambayo huadhimihwa kila ifikapo Machi 15, na mwaka huu Kauli mbiu ni usawa wa huduma za fedha kigitali.

"TCRA itaendelea kuratibu mikutano ya namna hiyo ili kuweza na pokea na kutatua changamoto za watumiaji na watoaji wa huduma za mawasiliano nchini,"Alisema.

Kwa upande wake Meneja wa kitengo kinachoshughulikia Wateja kutoka TCRA Thadayo Ringo,aliwataka wananchi kuendelea kufanya uhakiki wa matoleo mapya ya simu wanazotumia pamoja na 'application' wanazozipakua ili kuepuka changamoto ya matumizi ya bando kuisha kwa haraka.

Ringo alisema TCRA inaendelea kuelimisha jamii kuhusu wizi wa mtandaoni na aliwataka wananchi kujiadhari na njia za mkato ikiwemo kudanganywa katika mashindano mbalimbali kwa kuambiwa umeshinda kiasi fulani cha fedha akiwa haujashiriki.

" Tujiadhari na njia za mkato hizo ndiyo zinasababisha watu wanatapeliwa, kwa mfano mtu unaambiwa umeingia katika shindano fulani ambalo ujawahi kushiriki au kucheza tuwe makini"àlisema


Aidha baadhi ya wadau wa mawasiliano walioshiriki katika mkutano huo wameiomba serikali kuondoa tozo ambazo zimekuwa zikileta vikwanzo katika utaoji huduma.

Mkurugenzi wa Leseni na Ufuatiliaji  wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) John Daffa akizungumza katika mkutano wa wadau kuelekea  Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mteja Duniani ambayo hufanyika kila Machi 15 kila mwaka uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Leseni na Ufuatiliaji  wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) John Daffa akijibu maswali ya wadau  katika mkutano wa wadau kuelekea  Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mteja Duniani ambayo hufanyika kila Machi 15 kila mwaka uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja wa kitengo kinachoshughulikia Wateja wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Thadayo Ringo akizungumza wakati akimkaribisha Mgeni rasmi katika kuelekea maadhimisho ya siku mtumiaji wa huduma za mawasiliano ,jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa Chuo Kampala Aalliyah George akizungumza kuhusiana na huduma za mawasiliano nchini zilivyoboreshwa na kwa wadau kutoa maoni ,jijini Dar es Salaam

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...