KATIKA kuendeleza utamaduni wa kuishirikisha jamii inayotuzunguka, Meridianbet kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
iliandaa shughuli maalumu ya kusafisha fukwe ya Coco Beach.
Coco Beach ni miongoni mwa fukwe pendwa na maarufu jijini Dar es Salaam, kwa
msingi huo, ni muhimu eneo la fukwe hii kuwa safi na salama kwa watumiaji ambao
wengi wao ni wafanyabiashara pamoja na wageni wanaotembelea eneo hilo kama
sehemu ya burudani na mapumziko.
Kwa
umuhimu na upekee wa fukwe hii, Meridianbet iliona ni muhimu kuandaa zoezi
maalumu la kuishirikisha jamii na serikali katika kuendeleza juhudi za
kusafisha na kupendezesha jiji la Dar es Salaam. Zoezi hili lilikua mahususi
kwa ajili ya usafi na usalama wa fukwe hii ambayo inatajwa kama fukwe pendwa
miongoni mwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
Ni
desturi iliyojengeka kwa Meridianbet kushiriki katika shughuli za kijamii na kuchangia kwa kile
kinachowezekana. Safari hii, Meridianbet
ilichangia vifaa vya usafi ikiwemo mafagio, mifuko maalumu ya kuhifadhia
takataka pamoja na vilinda mikono kama sehemu ya kuhakikisha zoezi la usafi
linakua endelevu kwenye fukwe hii. Pia, katika kuwatambua wafanyabiashara
ndogondogo ambao wengi wao ni wauza mihogo kwenye fukwe hii, Meridianbet iliwapatia mavazi maalumu kwa lengo la kuongeza unadhifu na usafi
wao pindi wanapokuwa kwenye shughuli zao.
Akishiriki
kikamilifu katika tukio hilo, Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makalla, ameendelea kutoa wito kwa wananchi kufanya usafi kwenye maeneo
yao huku akiwasisitiza wakandarasi kuhakikisha wanaondoa taka kwa wakati
kwakuwa tayari wananchi wamehamasika kufanya Usafi. Pia, ameipongeza na
kuishukuru kampuni ya Meridianbet kwa kujumuika na jamii ikiwa ni ishara ya kuunga mkono kampeni ya
Safisha, pendezesha Dar es Salaam yenye lengo la kuhamisha ufanyaji wa usafi
sehemu zote za jiji hili.
Hakika, Meridianbet Ipo Nawe Mahali Popote, Wakati Wowote!
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...