****************

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

Umoja wa wasanii wanawake Tanzania (UWAWATA) unaoongozwa na Mwenyekiti Hidaya Njaidi wamejitokeza kumuunga mkono diwani viti maalum Kibaha Mjini,Lidya Mgaya katika umaliziaji wa ujenzi wa nyumba ya watoto yatima huko mtaa wa Bamba,kata ya Kongowe.

Umoja huo umetoa msaada wa mabati,misumali na mbao (zaidi ya laki mbili).

Njaidi alisema kutoa ni moyo,na kudai watoto yatima ni watoto wa kila mmoja wanahitaji kusaidiwa.

Nae diwani viti maalum, Kibaha Mjini Lidya Mgaya ambae pia ni muhasibu wa umoja huo, alieleza amejitolea kujenga nyumba ya watoto yatima wanne ,na Bibi yao wa miaka 80 ambao maisha yao yanaendeshwa na kaka yao ambae amefeli kidato cha nne kwa kuelekeza akili kusaidia familia hiyo.

Lidya anajenga nyumba hiyo ambapo anashirikiana na wadau mbalimbali ili kufanikisha lengo lake.

Akiwa katika eneo la ujenzi Lidya alisema Faida Hamis Ramadhani, Mohamed Hamis Ramadhani, Selemani Hamis Ramadhani na, Sofia ni ndugu ambao wazazi wao wamefariki na kubaki na bibi mzaa mama yao ambae nae ni kikongwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...