Na CHRISTOPHER LISSA
UMOJA wa Wanawake Tanzania (UWT) , Kata ya Makongo, umeanza kufanya tathimini ya kina kuhusu mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na  Halmashauri ya  Manispa ya Kinondoni katika kata hiyo.

Akizungumza, Dar es Salam,  wakati Kamati ya Utekelezaji ya umoja huo Kata ya Makongo Juu  ilipokutana na  Ofisa Maendeleo kata hiyo, Mwenyekiti wa UWT wa  kata hiyo, Abbriaty Kivea,  alisema  lengo ni kujiridhisha na maendeleo ya utoaji na urejeshaji wa mikopo hiyo.
“Tunafanya tathimini hii ili kujua ni vikundi vingapi vilipata mikopo, marejesho na changamoto zilizopo ili tuweze  kuboresha  zaidi na hatimaye mikopo hiyo iwanufaishe walengwa,”anasema  Abbriatyy.

Anabainisha , UWT  Kata ya Makongo,  ina dhamira ya kuhakikisha mikopo hiyo inawafikia walengwa wengi   hususan wanawake, vijana na watu wenye ulemavu  na kuondoa malalamiko yaliyopo.

“Habari njema ni kwamba,  Kata ya Makongo itaanza kutoa mikopo mikubwa  zaidi kwa wajasiriamali  tofauti na  ya awali. Hiyo ni katika kutekeleza maelekezo ya Rais Samia  Suluhu Hassan. Tutatoa mikopo hiyo kwa vikundi vya watu watano watano,”anaeleza  Abbriaty.
Mwenyekiti huyo wa UWT anabainha , tayari vikundi 15 vimejitokeza kuomba mikopo  hiyo mikubwa  ambapo kikundi  kimoja  kimeomba kupatiwa sh. milioni 120 kwaajili ya kuendesha mradi wa kilimo cha pilipili.

Anasema  kati ya vikundi hivyo kikundi kilichoomba mkopo wa chini zaidi  ni sh. milioni 3.5 hali  inayoonyesha wazi  mikopo hiyo isiyo na riba  kuanza kumkomboa  mjasiriamali  mdogo kuwa mjasiriamali wa kati.

“Kupitia mikopo hii mikubwa wajasiriamali katika Kata ya Makongo Juu  wananza kumiliki viwanda .Na hii ndiyo dhamira ya serikali yetu chini ya Rais Samia,”anaeleza.
Abbriaty anasema tathimini hiyo pia ni kutaka kujua  mwenendo wa urejeshaji fedha kwa vikundi viliyo kuwa vimekopa ambapo UWT  katika kata hiyo ilipokea malalamiko kwa wana vikundi kuwa baadhi vimefanya marejesho  lakini havipati mikopo.

“Kuna vikundi ambavyo  vimerejesha fedha na kubakiwa na madeni madogo , hivi tunaomba vikopeshwe tena. Visikwamnishwe na watu wachache waliopo ndani ya vikundi hivyo. Pia kuna wengine wanadai wamerejesha fedha lakini wanadaiwa tena,”anasema.

Kwa upande wa Katibu wa UWT wa kata  hiyo, Deodatha Kommba, alisema tangu Januari mwaka huu , vikundi 18 vya wajasiriamali vimetambuliwa.

“Vikundi hivi vinaendelea kufanyiwa tathimini, kusajili  kisha kupewa mikopo kwani fedha bado zipo,”anaeleza  Benadetha.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...