Meneja huduma kwa wateja NSSF, Robart kidege akizungumza katika bonaza la michezo mbali mbali  lililofanyinika jijini Dar-es-Salaam
Mratibu wa bonanza , Nora Mwidunda akitoa shukrani kwa Mkurugenzi mkuu wa NSSF kwa kuruhusu michezo katika mfuko huo. jijini Dar es Salaam
Daniel Shaidi ambaye ni Afisa Mkuu Utawala kwa niaba ya Mkurugenzi wa Utawala, alisema michezo mbalimbali inayoendelea katika Mfuko ni muitikio wa NSSF wa kutekeleza muongozo wa Serikali uliotolewa mwaka 2014 ambao unazitaka taasisi za umma kushiriki katika michezo mbalimbali.

Na Mwandishi Wetu

Wakati wa kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 8, Wafanyakazi Wanawake wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wameshiriki bonanza la michezo mbalimbali.

Miongoni mwa michezo iliyofanyika katika bonanza hilo la kuvutia lililofanyika katika viwanja vya Chuo cha DIT jijini Dar es Salaam ni pamoja na mpira wa pete, mbio za kukimbiza kuku, mbio za magunia na mbio za riadha mita 200 na 400.

Akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, Meneja Huduma kwa Wanachama, Robart Kadege alisema katika kuelekea siku ya Wanawake Duniani, Mfuko ulishiriki shughuli mbalimbali za kijamii kwa kuanza kutoa msaada wa vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar pamoja na kufanya bonanza hilo la michezo ambalo lilishirikisha baadhi ya wafanyakazi wanawake wa NSSF.

Kadege alisema Mfuko unazingatia usawa wa kijinsia ambapo nafasi za uongozi zinatolewa kwa sifa bila ya kujali jinsia jambo ambalo litaendelea kufanyika na kuwahakikishia wafanyakazi kuwa haki ya usawa wa kijinsia katika Mfuko utaendelea kuwepo wakati wote na hiyo ni kuendana na kauli mbiu ya siku ya Wanawake  Duniani isemayo "Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu".

Naye, mratibu wa bonanza hilo, Nora Mwidunda, alisema wanamshukuru Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba kwa kuruhusu michezo kuendelea katika Mfuko huo na kubainisha kuwa timu ya mpira wa pete iko vizuri sanjari na michezo mingine kama mpira wa miguu, mpira wa wavu na riadha 'Jogging'.

Alisema Mfuko umepokea mwaliko wa michezo ya Siku ya Wafanyakazi 'Mei Mosi' ambayo kitaifa mwaka huu itafanyika mkoani Dodoma na itajumisha michezo ya aina mbalimbali.

Katika bonanza hilo timu nyekundu "Red Team" ilibuka kidedea katika mchezo wa mpira wa pete kwa kuiadhibu timu nyeusi "Black Team" kwa magoli 10 dhidi ya 8 na kukabidhiwa kitita cha shilingi 600,000 huku Black team ikijinyakulia zawadi ya shilingi 400,000. Nyota wa mchezo wa pira wa pete alikuwa mchezaji wa timu nyekundu Queen Msanya ambaye alijipatia zawadi ya shilingi 50,000.

Washindi wengine katika mchezo wa pete na zawadi walizopata kwenye mabano ni Sifa Kaitila ambaye alikuwa mchezaji bora (50,000) mzuiaji matata alikuwa ni Asha (50,000).

Kwa upande wa riadha, mshindi wa mita 400 alikuwa ni Juliana Haule ambaye alipata zawadi ya shilingi (200,000), mshindi wa pili alikuwa Mwanahawa Juma aliyepata zawadi ya shilingi (100,000) na Grace Ngalo ambaye ni mshindi wa tatu na alipata zawadi ya shilingi (50,000).

Washindi wa mbio za mita 200 na zawadi zao kwenye mabano, mshindi wa kwanza alikuwa Upendo (120,000) mshindi wa pili alikuwa ni Lucy (80,000) na mshindi wa tatu alikuwa ni Happy (50,000).

Kwa washindi wa mbio za magunia mshindi wa kwanza alikuwa ni Hadija ambaye alipata zawadi ya shilingi 300,000 mshindi wa pili alikuwa ni Dianess ambaye alipata zawadi ya shilingi 200,000 na mshindi wa tatu alikuwa ni Awena aliyepata zawadi ya shilingi 100,000.

Aidha, Maria Maro aliibuka mshindi wa mbio za kukimbiza kuku na kupata zawadi ya shilingi 100,000 pamoja na kuku huyo.


























Picha za Matukio mbalimbali yakiendelea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...