Na Jane Edward, Arusha

Uongozi wa chama Cha waigizaji Tanzania umetakiwa kuwasilisha wizarani ombi lao rasmi la kumwomba Rais wa jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kushiriki kongamano la kitaifa la chama Cha waigizaji linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Agizo hilo limetolewa na Naibu waziri wizara ya Utamaduni Sanaa na michezo Pauline Gekul wakati alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa chama Cha waigizaji wa filamu Tanzania unaofanyika kwa siku tatu jijini Arusha.

Gekul ametoa agizo Hilo kwa uongozi huo Mara baada ya chama hicho kutoa maombi ya kukutana na Rais Samia Suluhu Hasan katika risala yao iliyoisomwa na mwenyekiti kwa naibu waziri kuhusu kongamano la kitaifa wanalotarajia kulifanya .

Amesema kuwa kutokana na ombi la kumtaka Rais ashiriki kongamano la kitaifa anahidi kufikisha ombi Hilo kwa rais hivyo anaomba wawaailishe maombi ya tukio Hilo wizarani huku maombi hayo yakieleza tukio Hilo ni la lini na wapi na kuweka wazi agenda za mkutano Husika .

Aidha ameongeza kwa kuwataka waigizaji kuchangamkia fursa zinazotolewa na serikali ikiwemo mikopo inayotolewa na halmashauri kwa kuwa Ni kwa wananchi wote bila kuwepo ubaguzi.

Amedai kuwa mikopo inayotolewa sio ya ubaguzi hivyo wanapaswa kujiunga kwenye vikundi na kufuata tartibu za wanaosimania mikopo hiyo ili waweze kunufaika na fedha za serikali ambazo zitawezesha kuendesha shughuli zao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama Cha waigizaji wa filamu.nchini Tanzania Chiki Mchoma Akisoma risala yake kwa mgeni rasmi wameomba kutambuliwa na wizara ya utumishi na tamisemi kwa kuwa wizara hiyo Ni muhimu kwenye tasnia ya uigizaji na ndio inayoshikilia fedha zinazotokana na halmashauri site nchini.

Aidha Mchoma ameomba kuondolewa kwa Kodi na tozo za waigizaji kwani zimekuwa zikiwatesa na hivyo wanaomba wizara kuangalia namna ya kuwapunguzia kwa wakati angalau kwa miaka mitano ili kuwezesha vijana kuweza kuendesha shughuli zao za uigizaji.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...