Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

WAZIRI wa Katiba na Sheria George Simbachawene amewasilisha masuala mbalimbali yanayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa

Akizungumza leo Machi 23,2022 , Waziri Simbachawene ameanza kwa kushukuru na kueleza wamemaliza mkutano wa  Baraza la Haki za Binadamu uliofanyika katika Ofisi za Umoja wa Mataifa  Geneva  nchini Uswisi.

"Katika mkutano huo tumepata fursa ya kufanya mapitio  maalum ya vigezo mbalimbali kuhusu haki za binadamu,kila mwaka hufanyika tathimini ikiwa pamoja na uchambuzi wa maelekezo  mbalimbali yaliyokubaliwa na yale  hayajakubaliwa huwekwa kwenye rekodi ili yaendelee kutafakariwa

"Kwa hiyo nimefurahi kupata hii fursa ya kuweza kuzungumza kwenye baraza la Haki za Binadamu na Tanzania tumeeleza  hatua kubwa zilizochukuliwa katika mwaka huu mmoja wa uongozi na mabadiliko mengi yaliyofanyika katika masuala ya Haki za Binadamu  yanayohusiana na elimu,afya na demokrasia kwa ujumla

"Bila kusahau kwenye mkutano huo  tumegusia masuala ya maamuzi na utashi wa Rais wetu  Samia Suluhu Hassan ambaye aliruhusu mtoto wa kike aliyepata ujauzito baada ya kujifungua kuendelea na masomo,"amesema Waziri Simbachawene wakati akielezea yaliyojiri kwenye mkutano huo.


Kutoka Kushoto: Balozi Maimuna Tarishi, Mwakilishi wa Kudumu, Geneva, Mh. George Simbachawene Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Hoyce Temu Naibu Mwakilishi wa Kudumu Geneva na Nkasori Sarakikya Mkurugenzi Wizara ya Katiba na Sheria


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...