Na Mwandishi Wetu
Mhe. Samwel W. Shelukindo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Spain (mwenye makazi jijini Paris) ambaye pia ni Mwakilishi wa Tanzania kwenye Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO) ameshiriki kwenye Kikao cha Kwanza cha Dharura cha Baraza Kuu la UNWTO (First Extraordinary Session of the UNWTO General Assembly), jijini Madrid - Uhispania, tarehe 27 April 2022.
Kupitia kikao hicho, Nchi Wanachama wa UNWTO wamepitisha Azimio la kusimamisha uanachama wa Urusi kwenye Shirika hilo.
Kama ilivyoainishwa kwenye sera ya mambo ya nje ya nchi, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipiga kura ya kutofungamana na upande wowote kwenye rasimu ya Azimio hilo.
Mhe. Samwel W. Shelukindo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Uhispania mwenye makazi nchini Ufaransa akifanya mazungumzo na Bi. Elcia Grandcourt, Mkurugenzi wa Idara ya Kanda ya Afrika kwenye Shirika la UNWTO (kulia) jijini Madrid. Mazungumzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa 65 wa Kamisheni ya Afrika - UNWTO utakaofanyika Arusha, kuanzia Oktoba 5 hadi 7 mwaka 2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...