Mbeya,Tanzania

RPC Mkoa wa Mbeya Inspekta Urlich Matei amewahimiza bodaboda mkoa wa Mbeya kufanya malipo ya tozo za ushuru wa maegesho unaosimamiwa na wakala wa barabara wa vijijini na mijini TARURA,Zoezi hilo la tozo lilianza kutumik mkoani Mbeya April 1,2022.


RPC Matei pamoja na kutoa maelekezo hayo,alitoa msisitizo kwa bodaboda wote ndani ya jiji hilo kutii sheria bila shuruti,na kutojihusisha na vitendo vya uharifu.

Katika kikao hicho kilichoandaliwa na TARURA kwa kushirikiana na uongozi wa bodaboda mkoani Mbeya kwa lengo la kutoa elimu kwa bodaboda mkoani humo kuhusu mfumo wa kulipia maegesho kidigitali unaojulikana kama TeRMIS,wataalamu wa TARURA wamewaelimisha na kutatua changamoto zilizojitokeza tangu kuanza kwa mfumo huo mkoani Mbeya

OCD wa Mbeya Mjini kamanda James Chacha amewahamasisa bodaboda kuwa chachu ya maendeleo kwa kulipia ushuru wa maegesho, kwani unapolipia kutumia mfumo wa TeRMIS fedha inaenda serikalini na kuchangia shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara.

Aidha OCD Chacha pia amewasihi TARURA kuwapatia ushirikiano bodaboda pale tatizo linapojitokeza

Huu ni mwendelezo wa utoaji elimu kwa watumiaji wa vyombo vya moto na kuwaelimisha namna mfumo huo unavyofanya kazi.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...