*Umri Ni Namba Tu, Uwezo
Unaonekana!
Ilikua ni wikiendi bomba kwa wanafamilia ya Meridianbet ambao, waliandaa bonaza kabambe la kuwakutanisha maveterani wa
mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. Lengo kuu likiwa ni kuendelea
kudumisha utamaduni wa kufanya mazoezi kupitia michezo mbalimbali, soka ukiwa
ni mchezo unaopendwa na sehemu kubwa ya jamii zetu.
Bonanza la mwezi Aprili lililenga kuwakutanisha maveterani wa kitaa ambao, timu zao zilipendekezwa kwa wingi zishiriki tukio hili ambalo lilitangazwa hadharani kupitia mitandao ya kijamii ya Meridianbet. Timu 4 zilizopendekezwa kwa wingi, zilipata nafasi ya kushiriki mtanange huu ambao ulichezwa ndani ya Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mchezo wa kwanza uliwakutanisha Majohe
Veterans vs Fire FC
ambapo, mchezo ulimalizika kwa ushindi wa magoli 2-0 kwa Fire FC. Mtanange wa
pili ulikua kati ya Meridianbet FC vs
Kilongawima Veterans, mchezo huu ulitawaliwa na matukio ya piga ni kupige
ambazo, magolikipa walikua na kazi za ziada kuzilinda nyavu zao ambazo
zilimaliza mchezo bila kutikiswa. Mikwaju ya penati ikatumika kumsaka mshindi
na ndipo, Meridianbet
FC walipoibuka
kidedea kwa penati 5-4.
Mchezo wa kumsaka mshindi wa 3 uliwakutanisha Majohe vs
Kilongawima na
maveterani wa Majohe kuibuka kidedea kabla ya mchezo wa kumsaka bingwa wa
bonanza kati ya Fire FC vs Meridianbet
FC kuzichakaza nyavu.
Kwa mara nyingine, mikwaju ya penati iliamua bingwa kati ya Fire vs
Meridianbet ambapo, Fire
waliibuka kidedea kwa penati 6-5. Hakika, wikiendi ilifana kwa burudani
iliyotelewa na timu hizi ambazo zilikua na mashabiki wao uwanjani.
Kama ilivyokawaida ya Meridianbet, washindi walizawadiwa jezi na mipira ikawe sehemu ya kuendeleza juhudi zao za kimichezo na kuimarisha afya zao. Pia, huu ni muendelezo wa Meridianbet kuishirikisha jamii katika masuala mbalimbali yanayoigusa jamii moja kwa moja.
Hakika, Meridianbet Ni Familia
Kubwa!!
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...