N.Vero Ignatus,Arusha
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa hakuna fedha ya Serikali iliyotumika kwenye uzalishaji na uzinduzi wa filamu ya Tanzania ya The Royal Tour
Akizungumza katika uzinduzi wa filamu hiyo Jijini Arusha Rais Samia amesema watanzania wote wamefanikisha kupatikana kwa filamu hiyo ambayo itaitangaza nchi duniani kwa kuwa na vivutio mbalimbali vya utalii
"Niichukue fursa hii kwa kuwashukuru Sana watanzania wote waliochangia kwenye jambo hili,wafanyabiashara na wengine wote, kazi yote imefanywa kwa michango ya watanzania, hatukutumia pesa ya Serikali".alisema Rais Samia
Rais Samia amesema kuwa katika filamu hiyo waneweza kuonyesha mambo mengi ambayo Watanzania wengi walikuwa hawayafahamu ikiwemo ghala kubwa ya PEMBE za Tembo,Faru walizozikamata na kuzihifadhi katika sehemu mbalimbali za nchi na Nchi jirani, iili iwe funzo kwa watu wote Ulimwengu kwamba uhalifu kwa wanyama unahitajika kuachwa Mara moja
"Ghala kubwa ya meno ya tembo pamoja na Faru ambapo PEMBE hizo zimekamatwa zikiwa zinakwenda magendo,siyo zote zimetoka Tanzania bali nyingine nchi jirani tumeonyesha ili watanzania waone na Ulimwengu wajue jambo hilo linaloendelea silo Tanzania tumekuwa wakwanza kuonyesha na kusema umati wa wanyama wanatejetea hivyo jambo hilo siyo vyema".alisema Rais Samia
Rais Samia amesema kuwa wakizungumzia nyota wa kweli katika filamu, hiyo bado inabakia kwa Watanzania wote, ambao ndiyo wamewezesha kufanikiwa kwa jambo hilo
Aidha Rais Samia amesema,wametangaza utalii na vivutio vilivyomo, kwaajili ya biashara ,hivyo mara baada ya kuonekana kwa filamu hiyo nchini Marekani ,idadi kubwa ya watu Ulimwengu, wameahidi kuja nchini Tanzania, kutokana na kuvutia na vivutio vya utalii nchini
Aidha filamu hiyo ya The Royal Tour zaidi ulifanyika uzinduzi tar 18/4 2022 nchini new york Marekani, 21/4 ikazinduliwa nchini Los Angel, 28/4 umefanyika uzinduzi wa kwanza uzinduzi wa kwanza nchini Jijini Arusha,baadae 7/5 Zanzibar na 8/5 Dar es salaam ambapo itaonyesha katika vituo vyote vya luninga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Arusha International Conference Centre AICC Jijini Arusha tarehe 28, Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya Heshima kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Eliya Mjatta kuthamini mchango wake katika Tasnia hiyo mara baada ya uzinduzi wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour Jijini Arusha 28, Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo pamoja Makamu Mwenyekiti wa CCM Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana wakiwa na wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia uzinduzi wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour Jijini Arusha 28, Aprili, 2022.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo pamoja Makamu Mwenyekiti wa CCM Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana wakiwa na wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia uzinduzi wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour Jijini Arusha 28, Aprili, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati akitoa misaada ya Vyakula mbalimbali pamoja na mafuta kwa vikundi 27 vya Watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi Mkoani Arusha tarehe 28, Aprili, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi mara baada ya kuwakabidhi msaada wa vyakula pamoja na mafuta kwa vituo mbalimbali 27 vya Watoto hao tarehe 28, Aprili, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwandishi wa Habari Maarufu wa Marekani ambaye ndiye mtayarishaji wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour Peter Greenberg mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Arusha International Conference Centre AICC Jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa Filamu hiyo tarehe 28, Aprili, 2022.

Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Arusha International Conference Centre AICC Jijini Arusha tarehe 28, Aprili, 2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...