Na Said Mwishehe, Tanga

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Shaka Hamdu Shaka amesema ziara ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tanzania Bara Abdulrhaman Kinana ina lenga kuwakumbusha wana CCM wajibu ukiwemo wa kuendelea kutatua changamoto na kero zinazowakabili wananchi.

Akizungumza mbele ya wana CCM wakiwemo viongozi wa ngazi mbalimbali za Mkoa wa Tanga leo Aprili 25, 2022, Shaka amesema kuwa Kinana ameanza ziara yake jana katika Mkoa wa Pwani na jana jioni aliingia Mkoa wa Tanga.

Pamoja na mambo mengine Shaka amewakumbusha wana CCM kwamba hivi sasa ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ya kuwasemea Watanzania wanatakiwa kwenda bega kwa bega badala ya ile misemo ya kwamba tuko nyuma yako.

“Huko nyuma tumekuwa tukiambiana tuko nyuma yako, lakini umefika wakati sasa kwa wana CCM badala ya kuwa nyuma yako basi tukawa bega kwa began a hii ndio njia nzuri itakayotuwezesha kutekeleza majukumu yetu kwa haraka.”Moja ya wajibu wa Chama chetu ni kuendelea kushughulikia masuala yanayohusu maendeleo ya makundi mbalimbali.”

Amewakumbusha wana CCM katika Mkoa huo kwamba bila CCM imara nchi yetu itayumba na kiongozi imara atatoka ndani ya Chama hicho huku akiwakumbusha moja ya malengo yao ushindi ni lazima na ili ushindi upatikane kuna mambo ya kufanyika kwa mujibu wa Katiba.

Shaka amesema moja ya mambo hayo ni uimarishwaji wa Chama na jumuiya zake , hivyo kila mmoja ajiulize amefanya nini katika kuimarisha Chama na jumuiya.Wakati jambo la pili ni ushirikishwaji na uwajibikaji katika kutambua kero na changamoto zinazowakabili wananchi.

“Katika hili la kutatua changamoto na kero za wananchi wamo viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo madiwani, wabunge na viongozi wa kitaifa lakini ili kufikia malengo ya kutatua kero hizo kwa haraka kila mmoja anayo nafasi ya kushiriki.

“Hapo katikati kumekuwepo na ombwe, hivyo niowambe wana CCM tutambue tuna kazi ya kufanya, na Tanga kwa takwimu zinaonesha Uchaguzi Mkuu uliopita tulishinda kwa asilimia 52 na ndio waliojitokeza kupiga kura, hivyo tujiulize ile asilimia 48 iliyobakia iko wapi .

“Hivyo kazi iliyobakia kila kiongozia awajibike katika kukisemea na kukitangaza Chama cha Mapinduzi na kwa kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan inafanya kazi ya kukisemea chama chetu kuwa rahisi,”amesema Shaka.

Aidha amesema dhumuni la ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM ni katika kuhakikisha wanaendelea kukumbusha kuhusu namna ya kukitumia chama hicho huku akifafanua kuwa wenye wajibu wa kuisimamia Serikali ni wana CCM hivyo waseme na watoe maelekezo.”Tuna kazi kubwa ya kuelekea 2024 na kuna kazi kubwa ya kuelekea 2025, huu ni wakati wa kujinga.”


KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Shaka Hamdu Shaka akizungumza mbele ya wana CCM wakiwemo viongozi wa ngazi mbalimbali za Mkoa wa Tanga leo Aprili 25, 2022, katika ukumbi wa Lembeni mjini Korogwe.Shaka amesema kuwa Kinana ameanza ziara yake jana katika Mkoa wa Pwani na jana jioni aliingia Mkoa wa Tanga.

 Baadhi ya wana CCM wakiwemo viongozi wa ngazi mbalimbali za chama sambamba na Wabunge wa mkoa wa Tanga wakifuatilia yalikuwa yakijiri ukumbini humo. PICHA NA MICHUZI JR-MMG.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...