Na Amiri Kilagalila,Njombe
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Ndugu.Sahili Geraruma ameagiza viongozi wa umma nchini kuacha kufanya kazi kwa nidhamu ya woga ili kazi zao ziweze kutekelezwa kwa ufanisi.
Geraruma ametoa agizo hilo wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe wakati akikagua na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika mitaa ya mji mdogo uliopo katika kata ya Ilembula.
“Ndugu zangu viongozi msifanye kazi kwa nidhamu za uoga kisa umeskia Mwenge unakuja ndio unafanya kazi usiku na mchana huko ni kuidhalilisha serikali”alisema Geraruma
Amesema serikali imewaamini viongozi wa umma hivyo ni wajibu wao kuonyesha uchapakaji kazi ili kuwaletea wananchi maendeleo.
“Serikali imetupa kazi,tuwatumikie wananchi na kama hutaki unasema kwasababu kuna watanzania wengi ambao wanaifanya kazi tunazozifanya na wanazihitaji,naagiza mkipewa kazi na serikali kuanzia ngazi ya chini hebu fanya kazi kwa moyo mmoja kwa kuwa wewe ndiye uliyeomba kazi”aliongeza Geraruma
Aidha mbio za Mwenge wa uhuru zimeukagua mradi huo na kuweka jiwe la msingi kutokana na kuridhishwa na namna mradi unavyojengwa.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...