Na.Khadija Seif, Michuzi TV
JAMII
imetakiwa kuwaonyesha upendo watoto waishio na virusi vya ukimwi Ili
kujiona wenye thamani na Haki ya kuishi na kuyafikia Malengo yao kama
watoto wengine.
Akizungumza
hayo Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima wanaoishi na virusi vya
ukimwi kilichopo fuoni Visiwani Zanzibar ,Abdul Majid amesema wakati
mwengine watoto hao wanachohitaji kwenye jamii ni upendo na Mapenzi.
"Jamii
haitakiwi kunyanyapaa watoto Hawa kwani bado Wana Haki ya kuishi na
Wana Haki ya kupendwa na kutimiza Malengo yao kama watoto wengine."
Hata
hivyo ametoa shukrani Kwa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) Kwa kufika
kituoni hapo na kugawa baadhi ya Mahitaji Kwa lengo la kusaidia watoto
hao .
Kwa upande wake
Meneja wa Shirika hilo Hamida Juma ametoa pongezi za dhati Kwa wizara ya
Maendeleo, jinsia na watoto kwa upande wa Visiwani Zanzibar kwa
kuwashika Mkono bega Kwa bega na kuhakikisha wanatoa misaada Kwa vituo
vya watoto yatima vinne.
Meneja wa Shirika la Bima la
Zanzibar (ZIC) Hamida Juma akiwa na viongozi wa Shirika hilo pamoja na
watoto yatima kutoka kituo kilichopo fuoni Visiwani Zanzibar mara baada
ya kupokea Mahitaji mbalimbali ikiwemo Mchele,Sabuni,Mafuta na Sukari
vilivyotolewa na Shirika hilo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...