Na Mwandishi wetu, Hanang'


WANAFUNZI 72 wa kidato cha sita wa shule ya sekondari Endasak Wilayani Hanang' Mkoani Manyara, wameahidi kufaulu kwa alama ya kwanza kwenye mtihani wao wa kuhitimu unaotarajiwa kufanyika mwezi Julai mwaka huu.

Wanafunzi hao 72 ambao wavulana ni 45 na wasichana ni 27 wanaosoma taasusi za fizikia, kemia na hisabati, uchumi, jiografia na hisabati wameahidi hayo kwenye mahafali ya pili ya kidato cha sita ya shule hiyo.

Mmoja kati ya wanafunzi hao Dora Kahise akisoma risala ya wahitimu hao amesema wanafunzi 98 walipangwa kujiunga na shule hiyo ila waliojiunga na shule hiyo ni 72.

"Tulipangwa 98 ila wanafunzi wengine 26 hawakujiunga kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuhama au kutoripoti kabisa shuleni," amesema Kahise.

Amesema kutokana na kumaliza mitaala mitatu badala ya minne na kusoma kwa malengo wamepata uzoefu hivyo wanatarajia kuhitimu kwa daraja la kwanza.

Mkuu wa shule hiyo Gisela Msoffe amesema shule imefanikiwa kuhamasisha wazazi kuwa karibu na wanafunzi ili kuleta matokeo mazuri kitaaluma.

"Hii ni baada ya mafanikio makubwa shule iliyopata mwaka 2021 kwa kufaulisha kwa asilimia 100 ikiwa ni pamoja na shule kuinuka kitaaluma," amesema Msoffe.

Amesema wanakabiliwa na ukosefu wa maktaba nzuri na ya kisasa, hivyo kutegemea darasa moja la kuweka baadhi ya vitabu na mitihani iliyopita.

Amesema huduma ya maji haikidhi mahitaji ya wanafunzi wote shuleni hapo na kusababisha baadhi ya huduma kukwama ikiwemo chakula, usafi na utunzaji wa mazingira.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...