*Waganga wa Kienyeji si wataalam lishe

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv

Wataalam wa lishe wametakiwa kufanya kazi kwa weledi ili kutoa elimu sahihi ya lishe kwani magonjwa mengi yasioambukiza yanatokana na ulaji usiozingatia lishe.

Hayo aliyasema Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mafunzo na Elimu ya Lishe wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC)Dk.Esther Nkuba wakati wa ufunguzi wa Mkutano Chama cha Wataalam wa Lishe Tanzania (TNDA) uliofanyika katika Ukumbi wa Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.

Dk.Esther amesema kazi ya chama hicho ni kusimamia taaluma yao katika kuhudumia wananchi ili waweze kujua lishe kutokana na vyakula vinavyowazunguka katika maeneo yao

Amesema takwimu za lishe zinaonyeshesha Tanzania kuwa aslimia 32 hivyo ni kazi ya wataalam kuendelea kutoa elimu ya kupunguza kwa kutoa elimu ya ulaji unaozingatia afya ya lishe bora.

Amesema mikoa yenye uzalishaji wa chakula kingi kama Iringa,Njombe,Ruvuma ,Mbeya,Rukwa ,Katavi pamoja na Tabora na ndio inaongoza kwa utapiamlo ambapo ni kazi ya wataalam wa lishe kutoa elimu ya lishe.

Amesema kuwa suala la lishe lina umhimu katika Taifa kwani uchumi unajengwa na watu wenye afya ya kufanya uzalishaji uchumi huo.

Aidha amesema wataalam wa lishe ni wakati umefika wa kufanya kazi ya kutoa elimu na sio kuwaachia waganga wa kienyeji kushughulika kutoa elimu wakati sio wataalam wa sekta hiyo.

Hata hivyo amesema TFNC itakuwa bega kwa bega kuendelea kuwashika wataalam wa lishe katika kujenga afya za wananchi katika suala lishe kuwa ni suala kila mmoja kujua.

Mwenyekiti wa Chama hicho Abubakari Mzee amesema kuwa wameamua kuwa na chama ili kuweza kutoa elimu ya lishe pamoja kujenga uwezo miongoni mwa wataalam wa lishe.

Amesema kuwa katika mkutano huo utatoa matokeo chanya katika kwenda kutekeleza masuala ya msingi yahusuyo lishe katika jamii

Aidha amesema kuwa chama kitasimamia masilahi ya wataalam wa lishe kuthaminiwa kwani ndio kiungo cha kufanya wananchi wanakuwa na afya bora.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo na Elimu ya Lishe wa  Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) Dk.Esther Nkuba akizungumza na waandishi ww habari mara baada ya kufungua mkutano wa Chama cha Wataalam wa  Lishe (TNDA)  uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti  wa Chama cha Wataalam wa Lishe Tanzania (TNDA) Abubakari Mzee akizungumza na waandishi habari kuhusiana na mikakati ya chama hicho katika utoaji wa elimu ya lishe wakati mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Wanachama wa TNDA wakifatilia mada wakati wa mkutano wa kwanza wa chama hicho .

Picha za Makundi mbalimbali ya wanachama wa TNDA mara baada ya kukutana katika mkutano wa kwanza jijini Dar es Salaam.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...