WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda mapema leo amezindua vitabu na vifaa maalum saidizi kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa shule za Tanzania Bara na visiwani.

Awali akikagua vitabu hivyo Mabibo Jijini Dar es Salaam, Prof. Mkenda alimpongeza Mkurugezi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na wadau wote katika kukamilisha mpango huo kabambe.


"Hongereni sana TET kwa kufanikisha mpango huu.

Kazi nzuri na nimeshuhudia vitabu na vifaa hivi hapa, nawapongeza sana na tuendelee kujipongeza kwa kazi hii ambayo Mhe Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akitaka kuona kila mmoja anafikiwa wakiwemo watoto wenye uhitaji maalum." Alisema Waziri Prof. Mkenda.

" vifaa na vitabu vya Kidato cha 1-6 vya Braille na Maandishi yaliyokuzwa kwa ajili ya mwanafunzi wenye mahitaji maalumu ya kutokuona na uoni hafifu nchini vilivyoandaliwa kupitia mradi wa mpango na matumizi ya fedha za maendeleo kwa ustawi na mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilipokea kiasi cha bilioni 64 kwa ajili ya mradi wa maendeleo kwa ustawi na mapambano dhidi ya UVIKO 19.

Kupitia mradi wa mpango huo, Wizara ilipokea jumla ya Shilingi 707,000,000/- kwa ajili ya kuchapa vitabu vya kiada kwa matumizi ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu." Alisema waziri Prof. Mkenda.

"Ninaomba kutumia nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kujali na kuthamini elimu ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Kwa kutumia fedha hizo kwa mara ya kwanza katika historia Wizara imeweza kuandaa vitabu vya sekondari vya maandishi ya Braille na yaliyokuzwa kwa matumizi ya wanafunzi ngazi ya elimu ya sekondari Kidato cha 1-6.

Fedha hii imeweza kuchapa jumla ya nakala 9,100 ya vitabu vya Braille vyenye jumla ya juzuu 32,140 pamoja na vitabu vya michoro mguso vyenye jumla ya juzuu 20,400.

Vitabu hivi ni maalumu kwa ajili ya wanafunzi wasioona.

Vilevile, Wizara imeweza kuchapa vitabu vya kiada vya Maandishi yalikuzwa nakala 60,283 kwa ajili ya wanafunzi wenye uoni hafIfu.


Vitabu hivi vimechapwa katika uwiano wa vitabu vitatu kwa mwanafunzi mmoja (3:1).

Vitabu, hivyo ni vya masomo ya Geography, Kiswahili, Civics, Agriculture, English, History, Biology, information and Computer Science na Mathematics.

Vitabu hivi vitawezesha wanafunzi wenye mahitaji maalumu ya uoni kujifunza kama ilivyo kwa wanafunzi wengine na kupata stadi na mahiri mbalimbali zitakazowawezesha kumudu changamoto mbalimbali katika tendo la kujifunza.

Pamoja na vitabu hivi vilivyotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita, Serikali hii vilevile imekuwa na mahusiano mazuri na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Kupitia mahusiano hayo serikali imepata msaada wa kuandaa na kuchapa vitabu kutoka shirika lililopo nchini Korea Kusini liitwalo "Siloam Center for the Blind" lenye ofisi zake ndogo mkoani Kilimanjaro.

" Shirika hili limeweza kuchapa vitabu vya kiada vya Breli kwa sekondari kidato cha 1-6 nakala 4,000 za masomo ya English, History, Geography, Fasihi na Lugha na Sarufi kwa uwiano wa vitabu vitatu kwa mwanafunzi mmoja (3:1).

"Pamoja na vitabu hivyo, Serikali kupitia Mpango huo wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19 pia imetoa Milioni 770,000,000 kununua vifaa Maalum na Saidizi 413 kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum walioko katika vyuo vikuu kumi na moja (11).

" Vifaa vilivyonunuliwa ni Bajaji 35 kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa viungo.

" Kompyuta 72 na digital voice recorder 68 kwa ajili ya wanafunzi wasioona kuweka programu ya AVDA na kuweza kutumika kama Kompyuta za kawaida. Pia imenunua mashine za kisasa za kidigitali za kuchapia maandishi ya kawaida kuwa ya Braille kwaajili ya wanafunzi wasioona yaani Embosser tano (5). ".

Aidha, serikali imenunua Tablets 175 kwa ajili ya kupakia kamusi ya Lugha ya Alama ya Tanzania kwa ajili ya wanafunzi viziwi na Audiometer 39 kwa ajili ya kupima kiwango cha usikivu kwa wanafunzi viziwi.

"Kwani mwanafunzi kiziwi kila baada ya miezi mitatu anatakiwa kupima kiwango cha usikivu.

Vitabu hivi vinakusudiwa kusambazwa kwa wanafunzi 3,677 katika shule 764 za wanafunzi wasioona na wenye uoni hafifu Tanzania Bara na Zanzibar.

Aidha, vifaa maalum na saidizi vitagawiwa kwa wanafunzi 364 wenye ulemavu wa viungo, wasioona na wenye uziwi wanaosoma katika vyuo vikuu 11.

"Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia inaahidi kuendeleza kazi nzuri ambayo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wanafunzi wenye mahitaji maalum wanapewa fursa sawa kwa kuwapatia mahitaji wezeshi ikiwemo vitabu na vifaa maalum na saidizi vitakavyo wawezesha kujifunza sawasawa na wanafunzi wengine kwa lengo la kuboresha ujifunzaji wao na kupata matokeo chanya.

"Naomba nichukue fursa hii kuutangazia umma kuwa, amoja na vitabu na vifaa tunavyogawa leo, Serikali ya awamu ya sita pia imefanya yafuatayo kuhusu elimu maalum:-

1. Ununuzi wa vifaa vya bilioni 4.5 kwa ajili ya Elimu ya Msingi na Sekondari ili kuimarisha ujifunzaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum;


2. Ujenzi wa Shule mpya 3 Maalum za mfano na Mabweni 50 kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa lengo la kuimarisha usalama wao na kuboresha ujifunzaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum;

3. Uzinduzi wa mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi 2021/2022-2025/2026 kwa lengo la kuongeza fursa ya upataji Elimu katika ngazi zote za Elimu;

4. Uzinduzi wa Miongozo ambayo inatoa fursa sawa na kujali ujifunzaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

" Miongozo hiyo ni mwongozo wa Chakula na Lishe Shuleni (2021) Mwongozo wa Ujenzi wa Miundo Mbinu ya Elimu (2021) na Mwongozo wa Kuwarejeswa Shuleni Wanafunzi Walioacha shule kwa sababu mbalimbali (2022).

"Lengo letu ni kuhakikisha wanafunzi wote wakiwemo wale wenye mahitaji maalum wanapata fursa pana ya kujifunza, wakiwa usalama na wanapata lishe bora ili kuongeza ari ya ujifunzaji na ufundishaji;

5. Kutoa million 86,0000 kwa ajili ya Kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaotoka katika kaya zenye kipato duni kwa kuwalipia ada wanafunzi 05 katika ngazi mbalimbali za Elimu,

kuwanunulia Vifaa saidizi wanafunzi 50 wenye ulemavu mbalimbali, kuwalipia BIMA wanafunzi wenye mahitaji maalum 128 na kuwasaidia fedha za kujikimu wanafunzi 08 kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wanajifunza na wanamaliza masomo yao bila changamoto;

6. Kuwajengea uwezo waalimu walioko kazini 1983 wanaofundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa lengo la kuboresha mazingira ya utoaji wa Elimu maalum na Jumuishi katika ngazi ya Msingi na Sekondari; na

7. Kutoa mafunzo ya TEHAMA kwa walimu wasioona na wenye Uziwi 405 kwa lengo la kuwafanya waendane na Sayansi na Teknolojia na kuboresha utendaji wao wa kazi.

"Ninaomba kutumia nafasi hii kuwahimiza walimu kuvitunza vitabu na vifaa ambavyo tunawakabidhi,

" Naomba kusisistiza kuwa vitabu na vifaa hivi visifungiwe makabatini, wanafunzi wapewe nafasi ya kuvitumia ili wapate maarifa stahiki sawa na wanafunzi wengine.

"Napenda kutumia nafasi hii kutoa wito kwa viongozi wa taasisi na wadau zinazojishughulisha na utoaji wa Elimu Jumuishi, ziendelee kushirikiana na Serikali kuhamasisha umuhimu wa elimu kwa watu wenye mahitaji maalumu.

Aidha, napenda kuziomba familia na wadau wa maendeleo waendelee kuona umuhimu wa kuchangia juhudi za Serikali katika kuwapatia huduma stahiki wanafunzi wenye mahitaji maalumu ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika mchakato wa ujifunzaji.


Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Lugoba, Kuruthumu Moshi akisoma kitabu cha nukta nundu wakati wa uzinduzi wa kazi ya Kusambaza vitabu vya Breli na Maandishi yaliyokuzwa pamoja na ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa vyuo vikuu uliofanyika leo Aprili 5,2022 Jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMG
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda akipokea akizindua baadhi ya vitabu vya Kidato cha 1-6 vya Braille na Maandishi yaliyokuzwa kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu ya kutokuona na uoni hafifu nchini vilivyoandaliwa kupitia mradi wa mpango na matumizi ya fedha za maendeleo kwa ustawi na mapambano dhidi ya UVIKO-19



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda akipokea baadhi ya vitabu vya Kidato cha 1-6 vya Braille na Maandishi yaliyokuzwa kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu ya kutokuona na uoni hafifu nchini vilivyoandaliwa kupitia mradi wa mpango na matumizi ya fedha za maendeleo kwa ustawi na mapambano dhidi ya UVIKO-19 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk. Aneth Komba.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda akipokea baadhi ya vifaa ikiwemo kmpyuta, digital voice recorder ikiwemo na mashine za kisasa za kidigitali za kuchapia maandishi ya kawaida kuwa ya Braille kwa ajili ya wanafunzi wasioona kutoka kwa
Mkurugenzi wa Elimu Maalum Wizara ya Elimu Dkt Magreth Matonyawakati wa uzinduzi wa kazi ya Kusambaza vitabu vya Breli na Maandishi yaliyokuzwa pamoja na ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa vyuo vikuu uliofanyika leo Aprili 5,2022 Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda akionesha moja ya Kompyuta  kati Kompyuta 72 na digital voice recorder 68 kwa ajili ya wanafunzi wasioona kuweka programu ya AVDA na kuweza kutumika kama Kompyuta za kawaida pamoja na 
Tablets 175 kwa ajili ya kupakia kamusi ya Lugha ya Alama ya Tanzania kwa ajili ya wanafunzi viziwi .

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda( wa sita kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wa Wizara hiyo wakionesha baadhi ya vitabu vilivyozinduliwa wakati wa uzinduzi wa kazi ya Kusambaza vitabu vya Breli na Maandishi yaliyokuzwa pamoja na ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa vyuo vikuu uliofanyika leo Aprili 5,2022 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda akimsikiliza Mkurugenzi wa Elimu Maalum Wizara ya Elimu Dkt Magreth Matonya kabla ya kuzindua Bajaji 35 kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa viungo.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda akizindua moja ya bajaji ambayo itatumika kwa walimu wenye mahitaji maalumu wakati wa uzinduzi wa kazi ya Kusambaza vitabu vya Breli na Maandishi yaliyokuzwa pamoja na ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa vyuo vikuu uliofanyika leo Aprili 5,2022 Jijini Dar es Salaam.

MBUNGE wa viti maalumu mkoa wa Iringa Mhe.Rose Tweve akishiriki kuzindua moja ya Bajaji kati ya Bajaji 35 zitakazotumika kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa viungo.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...