Na Avila Kakingo - Michuzi TV

WIZARA ya Afya inampango wa kupunguza vifo vya watoto wachanga kutoka 20 kati 1000 kufikia vizazi hai 15 kati ya 1000 ifikapo mwaka 2025 huku ikiweka mkakati pia wa kupunguza visa vya watoto waliozaliwa wafu kutoka 16 kati ya 1,000 kufikia visa 12 kati 1,000 ifikapo mwaka huo.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Kaimu Mkurugenzi kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Afya, Catherine Sungura amesema huduma za afya kwa watu wote zinahitajika katika ngazi zote ikiwa ni Zahanati kila Kijiji, Kituo cha Afya kila Kata na Hospitali kila Wilaya.

Kuhusu vifo vya watoto amesema Wizara inampango wa kupunguza vifo vya Watoto chini ya miaka 5 kutoka 50 kati 1,000 hadi kufikia Watoto 38 kati 1,000 ifikapo 2025.

Wakati katika mimba za Utotoni Wizara inampango wa Kupunguza mimba za utotoni kwa wasichana walio na umri kati ya 15 hadi 19 toka asilimia 27 ya sasa kufikia asilimia 20 ifikapo mwaka 2025.

Akizungumzia Mkakati wa Pamoja wa Huduma za Mama na Mtoto No. 3 Sungura amesema kwamba Wizara ya afya inampango wa Kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kutoka 250 kati100,000 kwa sasa kufika 100 kati ya 100,000 ifikapo 2025.

"Kupunguza visa vya maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua kutoka 8% kufikia 2% ifikapo 2025." Amesema Catherine.

Amesema kuwa Wizara inavipaumbele vya Kuboresha Huduma, Matibabu, Dawa na Huduma kwa Mteja ili kukidhi mahitaji yanahihitajika na Mgonjwa ama mteja.

Aidha amesema wizara inafanya maboresho katika miundombinu, vifaa na vifaa tiba, kutoa mafunzo kwa Watumishi, Kusimamia miradi ya IMF, Kupambana UVIKO -19 pamoja na Kusimamia upatikanaji wa Sheria na Sera ya BIMA ya Afya kwa Wote.

“Katika kuboresha huduma za afya Wizara inampango wa Ujenzi wa Hospitali za rufaa za mikoa nane na za mikoa tano ambazo zitakuwa katika mikoa ya Njombe, Geita, Simiyu, Songwe na mikoa mingine ni Mara, Singida, Shinyanga mpaka kufikia mwaka 2025.”

Amesema kuwa katika Mkakati wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka 5 No.3
Hospitali ya Rufaa kila Mkoa na Huduma za Kibingwa kila Kanda zinahitajika.

Pia amesema kwamba na mkakati wa Sekta ya Afya wa Miaka 5 kuanzia mwaka 2021 hadi mwaka 2026 wizara itahakikisha wanawaweka wadau wa sekta pamoja ili kuchangia katika uratibu wa kutoa huduma za afya kwa ufanisi zaidi.

Catherine amesema kuwa lengo la Wizara hiyo ni kutoa huduma bora kwa kila mtu bila kujali hali na eneo alilopo. Wizara pia inampango wa Kupambana na magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza, Kuboresha huduma za utafiti, ubunifu na uwekezaji katika sekta ya afya.

Katika upatikanaji wa dawa na vifaa vya dawa na vifaa tiba amesema wataongeza bajeti ya huduma za afya ambayo ni endelevu kiuchumi.

Amesema maboresho ya Ujenzi wa vituo vya afya vyuo wizara itahakikisha itafanya ukarabati na kuhakikisha hospitali 67 za wilaya zinajengwa hadi kufikia 2025."Hospitali za kanda mbili zilizojengwa ifikapo 2025 ambazo zitakuwa katika mikoa ha Mtwara na Kigoma.”

Akizungumzia Ujenzi wa viwanda vya dawa na vifaa tiba amesema wizara inajitahidi kupunguza kuagiza nje dawa kwaajili ya kuhifadhi 'kusave' fedha za kigeni
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Afya, Bi. Catherine Sungura akizungumza wakati wa kikao kazi kati ya Wizara na waandishi wa habari kujadiliana na kushauriana masuala ya habari ili jamii izidi kupata taarifa zaidi kuhusu afya. Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, wakiwa katika kikao kazi kati ya Wizara ya Afya na waandishi wa habari, katika kikao hicho waandishi wa habari walijengewa uelewa kuhusu mikakati na vipaumbele vya Wizara ya Afya katika kuwahudumia wananchi.Kikao hicho kiliandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini -Wizara ya AfyaMwenyekiti wa waandishi wa habari waliohudhuria kikao kazi hicho Vincent Kasambala kutoka Upendo Media akizungumza jambo katika kikao kazi hicho kilichowakutanisha waandishi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam.

 

 

Mwandishi wa ITV, Richard Steven akiwasilisha maoni yaliyotolewa na kundi B, wakati wa kikao kazi kati ya Wizara ya Afya na waandishi wa habari, kilichosimamiwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo, Catherine Sungura, lengo ikiwa kujadiliana na kushauriana wapi Kitengo hicho kifanye maboresho ili jamii izidi kupata taarifa zaidi kuhusu afya.

Mkurugenzi wa FullShangwe Blog, John Bukuku, akichangia jambo wakati wa kikao kazi kati ya Wizara ya Afya na waandishi wa habari, kilichoandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano SerikaliniMwandishi wa masuala ya afya na jamii wa Matukio na Maisha Blog, Veronica Mrema akiwasilisha maoni yaliyotolewa na kundi A, wakati wa kikao kazi kati ya Wizara ya Afya na waandishi wa habari, kilichosimamiwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo, Catherine Sungura, lengo ikiwa kujadiliana na kushauriana wapi Kitengo hicho kifanye maboresho ili jamii izidi kupata taarifa zaidi kuhusu afya.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...