Na Amiri Kilagalila,Njombe

Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe kimekabidhi vyeti vya pongezi kwa vijana (UVCCM) takribani 130 wa wilaya ya Njombe kwa kufanikiwa kukaa pamoja kwa siku saba na kupata mafunzo mbali mbali yakiwemo ya uzalendo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vyeti hivyo,katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe bwana Erasto Ngole aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga kambi hiyo,ameagiza vijana hao kwenda kuonyesha uzalendo wao kwa vitendo ikiwemo kuhamasisha wananchi kwenda kushiriki shughuli za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa utakaofanyika uwanja wa saba saba mjini Njombe.

“Nimeshiriki makambi mengi kuanzia ya tawi mpaka taifa na kijana yeyote aliyepita kwenye kambi,akafundishwa uzalendo na kuiva huwa hawezi kukengengeuka kwa hiyo nina amini mnarudi vijijini na kwenye matawi yenu mkiwa tofauti na mlivyokuja”alisema Ngole

“Kesho nchi nzima itakuwa Njombe,maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge yamekamilika kwa kiwango cha kimataifa twendeni tukahimize watu na tukawashe Mwenge kwasababu tumepata fursa kubwa sana watu wa Njombe”aliongeza Ngole

Kwa upande wake mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Njombe Betreace Malekela ambaye ndiye aliykuwa akisimamia kambi hiyo amesema miongoni mwa mambo makubwa waliojifunza vijana hao ni pamoja kuipenda nchi yao.

“Vijana hawa wamejifunza vitu vingi ikiwemo pia miradi mbali mbali inayotekelezwa kwenye maeneo yao wakaona ni vema waungane pia kwa pamoja kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa tunapozungumzia miradi vijana hawa ndio wanufaika zaid”Alisema Betreace

Aidha Betreace amesema ikiwa leo ni siku moja kabla ya zoezi la uzinduzi wa mbio za Mwenge mkoani humo ,vijana hao wamekubaliana pia kuendelea kufanya hamasa ili kuhimiza wananchi kujitokeza katika uwanja wa Sabasaba.

Mariam Ng’olo na Hosea Mangula ni miongoni mwa vijana walioshiriki kambi hiyo imewasaidia kuwaunganisha na kujifunza vitu vikubwa wanavyokwenda kuvifanyia kazi ili kulisaidia taifa lao.

Katibu wa siasa na uenezi (CCM) mkoa wa Njombe akizungumza na vijana waliotunukiwa vyeti.
Baadhi ya vijana waliokuwa katika kambi wakifurahia mziki pamoja na katibu wa saiasa uenezi CCM mkoa wa Njombe bwana Erasto Ngole

 
Katibu wa siasa na uenezi akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki wa kambi hiyo ya vijana iliyokuwa katika ukumbi wa turbo mjini Njombe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...