Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda ameishukuru Benki ya NMB kwa kushiriki na kudhamini maonesho ya Kitaifa ya wiki ya ubunifu iliyoanza katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.



Maafisa wa NMB katika picha ya pamoja wakiwa kwenye banda lao, wakati wa maonesho ya Wiki ya Ubunifu yanayoendelea jijini Dodoma.

…………………………………..

Profesa Mkenda aliongezea kuwa, benki hiyo imekuwa karibu na wizara hata katika utoaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi kuanzia ngazi ya Diploma mpaka shahada za juu hivyo kusaidia wanafunzi wengi kujiunga na vyuo kuanzia mwaka ujao wa masomo.

“NMB sasa watatoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na tofauti ya kwao ni kuwa mikopo yao inatolewa kwa wanafunzi kuanzia Diploma hadi ngazi ya shahada,” alisema prof. Mkenda.

Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Kati, Nsolo Mlozi alimueleza Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar alipotembelea Banda la NMB, kuwa Benki ya NMB inathamini sana ubunifu na imekuwa ikiibuka na masuluhisho bora ambayo yamekuwa na manufaa kwa Benki na sekta ya fedha kwa ujumla.

“Tunathamini sana ubunifu kwani kwa kupitia hiyo, tumewaletea wateja wetu na watanzania kwa ujumla masuluhisho bora kama Mshiko fasta, lipa mkononi na NMB Pesa Wakala ambazo zinapunguza wingi wa wateja kufika matawini kupata huduma,” alisema Mlozi

Meneja huyo aliongezea kuwa, benki imeandaa fursa maalum kwa wabunifu mbalimbali hususani wabunifu wa masuluhisho ya kifedha kujaribu suluhishi zao za kiteknolojia kabla ya kuziingiza sokoni.

Maonesho ya kitaifa ya wiki ya Ubunifu yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolijia yameanza jana na yatamalizika Ijumaa ya tarehe 20 mwezi wa Tano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...